Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:14

Ramaphosa achaguliwa kiongozi mpya wa ANC Afrika Kusini


Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma akizungumza na makamu rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kabla ya mkutano mkuu, June 30, 2017.
Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma akizungumza na makamu rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kabla ya mkutano mkuu, June 30, 2017.

Chama tawala cha Afrika Kusini, ANC, kimemchagua naibu rais wa Afika Kusini Cyril Ramaphosa kama kiongozi wake mpya baada ya uchaguzi uliokua na ushindani mkubwa.

Uchaguzi huo unasemekana kuwa muhimu kabisa tangu chama tawala cha ANC kuchukua madaraka ya walio wengi chini ya Nelson Mandela miaka 23 iliyopita kutokana na mivutano ya ndani, rushwa na kupoteza umashuhuri wa chama hicho.

Ramaphosa, mwenye umri wa miaka 65, aliyewahi kuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi na baadaye kuwa mfanyabiashara na mmoja wapo wa matajiri wakuu wa Afrika Kusini, alimshinda mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamin Zuma mwenye umri wa miaka 68.

Wafanya biashara wamefurahia ushindi huyo na wachambuzi wanasema tangu habari kuanza kujitokeza soko la hisa la Afrika Kusini lilianza kupanda na sarafu ya Rand kuongezeka thamani yake kwa asili mia 3.

Kiongozi huyo mpya aliongoza kampeni ya kupambana na rushwa na kuahidi kuleta umoja katika chama baada ya mvutano wa muda mrefu na kupoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa zinazomkumba Rais Jacob Zuma.

XS
SM
MD
LG