Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 17:31

Kesi ya Zuma yaahirishwa


Former South African President Jacob Zuma in the dock at the High Court in Durban, South Africa, April 6, 2018.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefika mahakamani Ijumaa ambako kulikuwa na umati mkubwa wa watu akiwa anakabiliwa na tuhuma ya kesi ya muda mrefu iliyosababisha hasira kwa wananchi na hatimaye kupelekea kuondolewa kwake madarakani.

Wakati kesi ikisikilizwa iliochukua muda mfupi, Jaji Themba Sishi amesema Zuma alikuwa huru “lakini ajihadhari.”

Zuma, 75, alionekana mtulivu wakati jaji akitangaza kuwa kesi imeahirishwa hadi Juni 8.

Zuma ameendelea kusema kuwa tuhuma hizo dhidi yake zilikuwa zina msukumo wa kisiasa.

Baadae akitoka mahakamani katika mji wa Durban, alihutubia kikundi kikubwa cha wafuasi wake, wengi wakiwa wamevalia sare za chama cha ANC na wakiimba: “Zuma asiguswe.”

Wafuasi wa Zuma walikusanyika karibu na mahakama kueleza kuwa kiongozi huyo wa zamani hakuwa na kosa la udanganyifu, ulanguzi na wala kosa la kutakatisha fedha.

Baadhi ya wafuasi wa rais huyo walikuwa wamebeba mabango yalioandikwa “Fungeni mashirika ya wazungu yenye kumiliki kila kitu. Afrika ni ya Waafrika na Ulaya ni ya Wazungu.

Zuma ambae alijiuzulu Ijumaa Februari 14, alirithiwa na makamu rais, Cyril Ramaphosa, ambaye aliahidi kupambana na ufisadi na pia anataka kukijenga chama upya ambacho maadili yake yameporomoka tangia kilipochukua madaraka wakati utawala wa wazungu wachache ulipomalizika mwaka 1994.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG