Jimbo la Florida, hapa Marekani, limepitisha sheria mpya inayopiga marufuku utoaji mimba, baada ya wiki sita za ujauzito.
Jeshi la Israel Jumatatu limesema watu katika maeneo ya mashariki mwa mji wa Rafah wanapaswa kuelekea kwenye eneo ambalo jeshi limeliita eneo kubwa la kibinadamu ambalo linajumuisha Khan Younis, katika hatua ambayo inajiri kabla ya shambulizi lililopangwa la Israel huko Rafah.
Wabunge wa Marekani watapiga kura wiki ijayo, itakayobaini iwapo Spika wa baraza la wawakilishi Mike Johnson atasalia mamlakani, kwenye mojawapo ya nyadhifa za juu za uongozi katika serikali ya Marekani.
Hatua iliyoshangaza wengi ya kutangazwa kwa waziri mkuu mpya wa Haiti Jumanne, sasa inaligawanya baraza la mpito, lililoundwa hivi karibuni na kupewa jukumu la kuchagua viongozi wapya wa nchi hiyo ya Caribbean, yenye matatizo kutokana na uhalifu wa magenge.
Wamarekani wenye asili ya Asia ni kundi ambalo linakua kwa haraka sana lenye wapiga kura wanaostahiki nchini Marekani, kwa mujibu wa kituo cha utafiti cha Pew.
Kamanda mkuu wa kundi la Islamic State aliyekuwa akitafutwa kwa kuhusiana na vifo vya wanajeshi wa Marekani huko Niger wameuawa katika operesheni ilikuwa ikiendeshwa huko na wanajeshi wa Mali, jeshi la nchi hiyo limesema.
Sekta za Uchumi na uwajibikaji nchini Malawi vinaisihi serikali kushughulikia dosari katika mfumo wa ununuzi wa umma.
Afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya Marekani alionya Jumatatu kwamba zaidi ya watu milioni 2 katika mji wa El Fashir, katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan, wako chini ya tishio la "mauaji makubwa" kutokana na shambulio linalotarajiwa la kundi la wanamgambo la RSF.
Utani wa Rais wa Marekani Joe Biden ulipokelewa vyema na wale waliohudhuria chakula cha jioni cha waandishi huko White House Jumamosi usiku hapa Washington DC.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumatatu nchi yake inashughulikia kuongeza uwezo wake wa ndege zisizo na rubani - drones, wakati nchi hiyo ikipambana kuzima uvamizi wa Russia ulioanza zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Maafisa wa afya wa Palestina Jumatatu wamesema msururu wa mashambulizi ya anga ya Israel ya usiku kucha yaliua Wapalestina 22 katika mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wa Rafah.
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken amewasili Riyadh kwa ajili ya mazungumzo ya kikanda Jumatatu na Jumanne kuhusu msaada wa kibinadamu huko Gaza, mpango baada ya vita kwa maeneo ya Palestina, na utulivu na usalama katika Mashariki ya Kati.
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas alisema Jumapili kwamba ni Marekani pekee inayoweza kuizuia Israel kushambulia mji wa mpakani wa Rafah katika Ukanda wa Gaza.
Mchapishaji wa zamani wa gazeti la udaku David Pecker amerejea kizimbani kwa siku ya nne kama shahidi katika kesi ya uhalifu ya Donald Trump huko New York, Marekani.
Baraza Kuu la Mawasiliano la Burkina Faso (CSC) limetangaza kusimamisha matangazo na vipindi vya BBC/ Africa na VOA kufuatia habari iliyotangazwa kuhusu ripoti ya Human Rights Watch inayolishutumu Jeshi la Burkinabe kwa udhalilishaji mbalimbali wanaowafanyia raia.
Mfalme Charles wa Uingereza ametoa idhini yake kuwa sheria mpango wa Waziri Mkuu Rishi Sunak kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda.
Waziri mkuu wa Haiti anayeondoka madarakani Ariel Henry kupitia taarifa ya Jumatano amesema kuwa baraza la mpito litaapishwa Alhamisi kwenye afisi za Waziri mkuu iliyoko katika viunga vya mji mkuu wa Port-au-Prince.
Bhangi ni suala nadra la makubaliano katika Amerika iliyogawanyika kisiasa, huku ukusanyaji maoni ukionyesha kwamba asilimia 88 ya Wamarekani wanaunga mkono walau kwa kiasi fulani kuhalalisha bhangi.
Kenya imetoa tahadhari ya mafuriko wakati mvua kubwa zikinyesha katika eneo hilo. Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya limesema mafuriko katika taifa hilo la Afrika Mashariki yameua watu 38 na zaidi ya 11,000 wamekoseshwa makazi.
Mahakama ya Juu ya Marekani imepanga kipindi maalum kusikiliza hoja kama Rais wa zamani Donald Trump anaweza kushitakiwa kwa juhudi zake kutaka kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambapo alishindwa na Rais Joe Biden.
Pandisha zaidi