Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 05, 2024 Local time: 02:09

Asilimia 88 ya Wamarekani wanaunga mkono kwa kiasi fulani kuhalalishwa bhangi - Utafiti


FILE - Muuzaji wa bhangi anamrejeshea chengi mteja katika soko la bidhaa hiyo huko Los Angeles, Aprili 15, 2024.e
FILE - Muuzaji wa bhangi anamrejeshea chengi mteja katika soko la bidhaa hiyo huko Los Angeles, Aprili 15, 2024.e

Bhangi ni suala nadra la makubaliano katika Amerika iliyogawanyika kisiasa, huku ukusanyaji maoni ukionyesha kwamba asilimia 88 ya Wamarekani wanaunga mkono walau kwa kiasi fulani kuhalalisha bhangi.

Lakini watetezi wa bhangi wanasema hakuna mgombea hata mmoja wa juu wa urais anatumia mitazamo inayobadilika.

Takriban robo tatu ya Wamarekani wanaishi katika majimbo ambako bhangi ni halali kutumiwa kwa ajili ya matibabu. Nusu ya idadi ya watu wanaishi katika maeneo ambako bhangi inaruhusiwa kwa starehe.

Lakini Bhangi bado inaendelea kutizamwa kuwa si halali kwa mujibu wa sheria ya serikali kuu, ambako imewekwa pamoja na heroine na LSD kama dawa isiyo ya matumizi ya matibabu yanayokubalika kwa hivi sasa na kuna uwezekano mkubwa ikatumiwa vibaya.

Idadi kubwa ya wapiga kura wa Marekani ambao wanadhani kwamba ni vyema mabadiliko yafanyike kwa bhangi ni fursa muafaka kwa wagombea urais Joe Biden na Donald Trump, hasa miongoni mwa wapiga kura vijana, kwa mujibu ….. . … Scotty Smart, ambaye ni mratibu wa jumuiya katika kundi la kiraia la New Georgia Project.

Scotty Smart, New Georgia Project anaeleza: “Watu wengi hawaelewi sera. Watu wengi hawafahamu jinsi sera zinavyoathiri maisha ya kila siku. Nadhani banghi ni suala ambalo linachochea na kuwasisimua vijana wadogo kulipa mtizamo.”

FILE -Bhangi zinazotumika kama dawa inayotafunwa zikionyeshwa na kuuzwa katika Maonyesho ya bhangi ijulikanayo kwa jina la Kushstock huko Adelanto, California, Oktoba 20, 2018. (AP Photo/Richard Vogel)
FILE -Bhangi zinazotumika kama dawa inayotafunwa zikionyeshwa na kuuzwa katika Maonyesho ya bhangi ijulikanayo kwa jina la Kushstock huko Adelanto, California, Oktoba 20, 2018. (AP Photo/Richard Vogel)

Katika mkutano wa sera wa National Cannabis Festival and Washington mapema mwezi huu, muanzilishi Caroline Phillips alisema si Biden wala Trump alitimiza hilo.

Caroline Phillips, National Cannabis Festival amesema: “Kwa wote hao, jambo moja ambalo wanafana ni kwamba rekodi yao juu ya bhangi imekuwa haiendani na inaongezeka. Tumesikia ahadi kutoka kwa tawala zote mbili, hakuna hata moja ambaye amejitokeza wazi wazi.”

Chini ya Biden, Wizara ya Afya na Huduma za Binadamu impendekeza mabadailiko kuhusu bhangi na kuwa ni dawa nyepesi badala “kuiwekea upya’ uhalali wake ya kuifanya kuwa halali, ambapo itakuwa ‘kuiondoa katika orodha.’

Phillips anasema: “Sera ya sasa ya White House kuhusu bhangi haiko wazi. Wametupa ishara nzito kwamba wako tayari kufanya mabadiliko katika kuiweka katika kuiondoa, lakini kuna dalili kubwa itapangwa upya. Hata hivyo bado hatujaona hatua ya kuunga mkono maeneo yao.”

Mwaka 2018, rais wa wakati huo Trump alisema huenda ‘kwa hakika; angeunga mkono juhudi za kuondoa marufuku ya serikali kuu

Forum

XS
SM
MD
LG