Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 21, 2024 Local time: 05:38

Marekani yaeleza wasiwasi kikosi cha RSF huenda kikashambulia El-Fashir, Sudan


Balozi wa Marekani katika Umaoja wa mataifa Linda Thomas-Greenfield.
Balozi wa Marekani katika Umaoja wa mataifa Linda Thomas-Greenfield.

Afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya Marekani alionya Jumatatu kwamba zaidi ya watu milioni 2 katika mji wa El Fashir, katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan, wako chini ya tishio la "mauaji makubwa" kutokana na shambulio linalotarajiwa la kundi la wanamgambo la RSF.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Linda Thomas-Greenfield pia alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushinikiza pande zinazopigana kujizuia.

"Tayari kuna ripoti za kuaminika kwamba RSF na wanamgambo washirika wake, wameharibu vijiji vingi magharibi mwa El Fasher," Balozi Thomas-Greenfield aliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. "Na tunapozungumza, RSF inapanga mashambulizi hivi karibuni dhidi ya El Fasher," aliongeza.

RSF ni Kikosi kinachotawaliwa na Waarabu, kikundi cha wanamgambo ambacho kinaundwa na wapiganaji wa Janjaweed ambao walifanya mauaji ya halaiki huko Darfur mapema miaka ya 2000.

Mkuu wa RSF amekuwa kwenye mvutano wa kuwania madaraka kwa kutumia silaha na mkuu wa Wanajeshi wa Sudan kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Mapigano hayo yameenea kutoka mji mkuu wa Sudan, Khartoum, hadi maeneo mengine ya nchi, na sasa yanaonekana kuwa tayari kuikumba Darfur Kaskazini na raia walionaswa huko.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana faraghani kujadili hali hiyo Jumatatu na lilipewa taarifa na maafisa wa Umoja wa Mataifa wa kisiasa na kibinadamu.

Forum

XS
SM
MD
LG