Shirika hilo limesema limewaokoa watu 180 kutoka kwenye maji katika maeneo mbalimbali nchini.
Venant Ndigila, mkuu wa mipango katika shirika la kibinadamu huko Kenya, amesema mvua zimesabaisha majanga kwa Wakenya.
Misaada ya kibinadamu imejitokeza sana katika eneo hili. Na hili ni muhimu sana kuhusiana na malazi, ambapo familia hizo 11,275 …haziwezi kuzitumia nyumba zao, au zimepoteza nyumba zao” amesema Ndigila.
Kenya imeanza kupata mvua katikati ya mwezi Machi, lakini katika miezi michache iliyopita, mvua zimekuwa zikiongezeka kwa kiwango kikubwa.
Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya limesema zaidi ya milimita 100 za mvua zimerekodwa katika maeneo mengi nchini humo katika kipindi cha wiki iliyopita, na kusababisha vifo vya watu sita.
Forum