Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 21, 2024 Local time: 17:24

Kiongozi Islamic State aliyehusishwa na vifo vya wanajeshi wa Kimarekani auawa


Kambi ya jeshi ya Niamey 101 iliyoko Niamey huko Niger. Picha na BERTRAND GUAY / AFP.
Kambi ya jeshi ya Niamey 101 iliyoko Niamey huko Niger. Picha na BERTRAND GUAY / AFP.

Kamanda mkuu wa kundi la Islamic State aliyekuwa akitafutwa kwa kuhusiana na vifo vya wanajeshi wa Marekani huko Niger wameuawa katika operesheni ilikuwa ikiendeshwa huko na wanajeshi wa Mali, jeshi la nchi hiyo limesema.

Abu Huzeifa, anayejulikana na kama Higgo alikuwa kamanda wa kundi hilo linalojulikana kama Islamic State in the Greater Sahara.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza tuzo ya mpaka dola millioni tano kupata taarifa kuhusiana naye.

Huzeifa anaaminika kusaidia kufanya shambulizi mwaka 2017 kwa wanajeshi wa Marekani na wa Niger huko Tongo Tongo Niger, shambulio ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Marekani na wanne wa Niger.

Kufuatia shambulio hilo, jeshi la Marekani lilipunguza operesheni na washirika wa eneo hilo walioko Sahel.

“Utambulisho na uthibitisho umekusanywa kuthibitisha kifo cha Abu Huzeifa ama Higgo, gaidi wa nje anayejulikana sana,” jeshi la Mali lilisema katika taarifa ya Jumatatu jioni.

Moussa Ag Acharatoumane, kiongozi wa kundi lenye silaha la Tuareg linaloshirikiana na nchi hiyo amesema kwamba majeshi yake yanashiriki katika operesheni ambayo ilifanyika Kaskazini mwa mkoa wa Mali.

Picha ya Huzeifa iliyoonyeshwa katika kituo cha televisheni ya taifa ilimuonyesha akiwa katika amevaa nguo za jeshi na ndevu ndefu nyeusi na kushika bunduki mikononi mwake.

Mali imekuwa katika mapinduzi mawili ya kijeshi tangu mwaka 2020 wakati wa wimbi la machafuko ya kisiasa yaliyolikumba eneo zima za Afrika Magharibi na Kati.

Nchi hiyo imekuwa katika kipindi kibaya na mapambano yaliyokuwa yakifanywa na makundi ya wanajihadi linalohushwa na al-Qaida na kundi la Islamic State kwa zaidi ya muongo mmoja.

Forum

XS
SM
MD
LG