Njama ya Iran ya kumuua Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump inaonekana kumuhisisha raia wa Pakistani mwenye uhusiano na Tehran ambaye alitarajia pia kuwalenga wanasiasa na maafisa wengine wa juu.
Mvua kubwa imesababisha majengo kubomoka na kupelekea vifo vya watu 17 kaskazini mwa Sudan, huku nchi hiyo ikikabiliwa na mapigano ya takriban miezi 16 kati ya vikosi pinzani vya kijeshi, afisa wa afya ameliambia shirika la havari la AFP Jumanne.
China imepoteza mshirika baada ya kujiuzulu kufuatia shinikizo, kwa Waziri Mkuu wa muda mrefu wa Bangladesh, Sheikh Hasina, ambaye wakati wa ziara ya Beijing mwezi uliopita alitia saini mikataba 28 ya nchi mbili na kukubali kuongeza uhusiano kati ya nchi hizo na kuwa ushirikiano wa kimkakati.
Nia ya Rwanda ya kulinda maslahi yake dhidi ya Uganda ndiyo chanzo kikuu cha waasi wa M23 kuzuka tena hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, makundi mawili ya utafiti yanayohusiana na Chuo Kikuu cha New York yamesema katika ripoti ya Jumanne.
Rais Joe Biden wa Marekani, alijadiliana kuhusu mvutano wa Mashariki ya Kati na timu yake ya usalama wa taifa na Mfalme Abdullah II wa Jordan, Jumatatu.
Maporomoko ya ardhi na mafuriko yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 150 kote nchini China katika miezi miwili iliyopita huku dhoruba za mvua zikiikumba eneo hilo.
Marekani imekuwa ikizitaka nchi kupitia ushirikiano wake wa kidiplomasia kuiambia Iran kwamba kuongezeka kwa mvutano Mashariki ya Kati sio maslahi yake, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller amesema Jumatatu.
Takriban wanajeshi watano wa Marekani wamejeruhiwa katika shambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi nchini Iraq, Jumatatu, maafisa wa Marekani wameliambia shirika la habari la Reuters.
Makatibu watano wa majimbo ya Marekani wanamsihi mmiliki wa mtando wa X, Elon Musk kurekebisha program ya Akili Mnemba ya “chatbot” kwenye mtandao wa X, wakisema katika barua iliyotumwa Jumatatu kwamba imeeneza habari potofu za uchaguzi.
Makamu Rais wa Marekani, Kamala Harris ameripotiwa kuzindua uchaguzi wake kwa kumteua mgombea mwenza katika kinyang’anyiro cha urais 2024.
Maoni kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni yameonyesha wasiwasi Jumapili juu ya kuongezeka kwa idadi ya watu wanaokamatwa nchini Venezuela kufuatia uchaguzi wa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mashambulizi ya Israel Jumapili yameripotiwa kuuwa takriban watu 18 huko Gaza, wakiwemo wanne waliokuwa kwenye hema la wapalestina waliokoseshwa makazi ndani ya hospitali, wakati shambulizi ya kuchomwa visu lililofanywa na mpalestina mmoja likiuwa watu wawili mjini Tel Aviv.
Ripoti za Jumapili kutoka kwa maafisa wa serikali na vyombo vya habari vya Bangladesh zinasema kuwa ghasia mpya zilizotokea zimepelekea vifo vya zaidi ya watu 20, pamoja na kujeruhiwa kwa mamia wengine, kwenye makabiliano kati ya polisi, na wanafunzi pamoja na wanaharakati wa chama tawala.
Viongozi wa kidini pamoja na maafisa wa Olimpiki Jumapili wamekusanyika nje ya hekalu la Notre Dame mjini Paris, kuonyesha namna dini na spoti zinavyoweza kushirikiana, kulingana na mkuu wa Kamati ya Olimpiki Thomas Bach.
Katika ushindani wa urais, mgombea wa Republican Donald Trump na mgombea mtarajiwa wa Democratic Kamala Harris wote wako katika safari za kampeni, ambapo Trump alihoji utambulisho wa rangi wa Harris na Harris alitoa changamoto kwa Trump wafanye mdahalo.
Israel Alhamisi ilisema ilimuua kiongozi wa kijeshi wa Hamas Muhammad Dief, anayemaanika kuwa ndiye alipanga shambulizi la Hamas la Oktoba 7 dhidi ya Israel, katika mji wa kusini mwa Gaza wa Khan Younis katikati mwa mwezi Julai.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumatano alionya kwamba Israel kumuua kamanda wa Hezbollah mjini Beirut na mauaji ya kiongozi wa Hamas mjini Tehran yanaashiria “uzidishaji hatari” wa hali ya taharuki huko Mashariki ya Kati.
Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh aliuawa mjini Teheran Jumatano, kulingana na taarifa tofauti zilizotolewa na Hamas na kikosi cha ulinzi cha Iran.
Jeshi la Israel Jumanne jioni lilisema lilifanya shambulizi mjini Beirut likimlenga kamanda wa Hezbollah ambaye linadai alihusika na shambulio la anga ambalo liliua watoto 12 na vijana waliokuwa wanacheza kwenye uwanja wa mpira mwishoni mwa juma katika milima ya Golan.
Rais wa Marekani Joe Biden, wakati kukisalia miezi sita katika utawala wake, Jumatatu alitangaza mapendekezo kadhaa ya kufanya marekebisho kwenye Mahakama ya Juu ya Marekani, akiomba majaji tisa wa mahakama hiyo wawe na muhula wa miaka 18 badala ya muhula wa maisha yote.
Pandisha zaidi