Waziri wa ulinzi Yoav Gallant alimtaja Deif kuwa “Osama bin Laden wa Gaza”, akimaanisha Bin Laden aliyepanga shambulizi la 2001 la kundi la kigaidi la al-Qaeda nchini Marekani ambalo liliua karibu watu 3,000.
Gallant alisema kuuawa kwa Deif tarehe 13 Julai “ ni hatua kubwa katika mchakato wa kulisambaratisha kundi la Hamas kama jeshi na mamlaka inayotawala huko Gaza, na katika kufikia malengo ya vita hivi.”
Jeshi la Israel lilisema katika taarifa kwamba lilithibitisha kuwa Deif alikufa kulingana na tathmini ya kijasusi lakini halikutoa maelezo zaidi.
Israel ilikuwa imemlenga katika shambulizi lililoua watu 90, lakini hatma ya Deif haikujulikana.
Hamas haijathibitisha au kukanusha kifo chake.
Forum