Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 13:00

Rais Biden apendekeza muhula wa miaka 18 kwa majaji wa Mahakama ya juu


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden, wakati kukisalia miezi sita katika utawala wake, Jumatatu alitangaza mapendekezo kadhaa ya kufanya marekebisho kwenye Mahakama ya Juu ya Marekani, akiomba majaji tisa wa mahakama hiyo wawe na muhula wa miaka 18 badala ya muhula wa maisha yote.

Aliomba kuwepo pia sheria ya maadili kwa mahakama hiyo.

Aliomba pia marekebisho ya katiba ambayo yatapiga marufuku kinga kamili kwa marais ya kutoshtakiwa kwa makosa ya jinai ambayo wanaweza kuwa wamefanya wakiwa madarakani baada ya muhula wao kumalizika.

Pendekezo hilo la Biden ni kukemea uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Juu uliompa Rais wa zamani Donald Trump na marais wote wajao kinga dhidi ya kushtakiwa kwa vitendo vyao rasmi lakini sio kwa vitendo visivyo rasmi.

Biden alisitisha kampeni yake ya kuwania muhula wa pili wiki moja iliyopita na hatapata fursa ya haraka ya kutekeleza marekebisho hayo kwenye Mahakama ya Juu.

Biden alitangaza mapendekezo hayo katika hotuba katika Maktaba ya Rais ya Lyndon B. Johnson na Jumba la makumbusho huko Austin Texas, wakati wa kuadhimisha miaka 60 ya sheria ya haki za kiraia nchini Marekani ambayo inahakikisha Wamarekani wote wana haki ya kupiga kura na kujaribu kukomesha ubaguzi wa rangi, dini au asili ya kitaifa.

Forum

XS
SM
MD
LG