Wakati huohu0 Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akionya kwamba Iran na washirika wake katika eneo hilo “watalipa gharama kubwa” endapo wataishambulia Iran.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amesema katika kikao na wanahabari Jumatatu kwamba Iran haina lengo la kuzidisha mvutano katika eneo hilo, lakini ina haki ya kuiadhibu Israel kufuatia shambulio la wiki iliyopita lililomuua kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyeh, mjini Tehran.
Iran inailaumu Israel kwa mauaji ya Haniyeh, ambayo yalifanyika saa chache baada ya shambulizi la anga la Israel mjini Beirut lililomuua kamanda wa kundi la wanamgambo wa Hezbollah, ambalo ni kama Hamas linaungwa mkono na Iran.
Forum