Mzozo umeendelea kutokota tangu kutokea kwa vita vya miezi 10 huko Gaza, pamoja na kuuwawa kwa viongozi wawili wa wanamgambo kwenye mashambulizi mawili tofauti nchini Lebanon, wiki iliopita. Mauwaji hayo yamezua vitisho kutoka kwa Iran pamoja na washirika wake, huku kukiwa na hofu ya ghasia hizo kuenea kikanda.
Magen David Adom kutoka timu ya uokozi ya Israel amesema kuwa watu waliochomwa visu mjini Tel Aviv ni mwanamke wa umri wa miaka 70 na mwanaume wa miaka 80, wakati wanaume wengine wawili wakiendelea kupokea matibabu hospitalini. Ripoti za polisi zimeongeza kusema kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na mwanamgambo wa Kipalestina ambaye pia aliuwawa mda mfupi baadaye.
Israel imekuwa ikijiandaa kwa shambulizi la kulipiza kisasi baada ya kuuwawa kwa kamanda wa ngazi ya juu wa Hezbollah wiki iliopita nchini Lebanon, pamoja na kiongozi wa Hamas, kwenye shambulizi lililofanyikia kwenye mji mkuu wa Iran. Viongozi hao wawili wanahushishwa na vita vya Gaza vinavyoendelea, na vilivyozuka kufuatia shambulizi la Hamas la Oktoba 7 nchini Israel.
Forum