Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 04:44

Mawaziri wa Uingereza wakutana na Waziri Mkuu wa Lebanon


Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy na mwenzake wa Ulinzi John Healey wamefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa muda wa Lebanon Najib Mikati na Spika wa bunge Nabih Berri mjini Beirut hivi leo, katika ziara yao huko Mashariki ya Kati.

Katika ziara ya kushtukiza, Lammy na Healey waliasili Beirut wakilenga kupunguza kuongezeka kwa mivutano ya kikanda.

Mauaji ya mkuu wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyeh mjini Tehran siku ya Jumatano na shambulizi dhidi ya kamanda wa juu wa Hezbollah Fouad Shukuru mjini Beirut siku ya Jumanne yanatishia kueneza mzozo huko Mashariki ya Kati.

Hakuna aliyedai kuhusu na shambulizi la Jumatano lakini mashaka yameiangukia Israel, ambao iliapa kumuua Haniyeh na viongozi wengine wa Hamas kutokana na shambulizi la kundi hilo la Oktoba 7 nchini Israel ambalo limechochea vita huko Gaza.

Kiongozi mkuu wa Iran ameapa kulipiza kisasi dhidi ya Israel.

Lammy na Healey walikuwa Qatar siku ya Jumatano katika ziara yao ya kwanza ya pamoja.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG