Mashambulizi ya Jumapili yalilenga kile jeshi la Israel lilisema yalikuwa maficho ya silaha za Hezbollah na miundombinu.
Lakini mashambulizi hayo hayakufikia lengo la kulipiza kisasi baada ya shambulizi la Jumamosi ambalo liliua zaidi vijana na watoto.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisafiri kurudi nyumbani mapema akitokea katika ziara nchini Marekani ili kukutana na baraza lake la usalama na kutathimini hali ilivyo.
Katika ujumbe wa Jumapili kwenye mitandao ya kijamii, waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant aliomboleza waathirika wa shambulizi la Majdal Shams akisema “Tutahakikisha Hezbollah, kundi linaloungwa mkono na Iran linawajibishwa kwa maafa hayo.”
Awali, Netanyahu alionya “Hezbollah itawajibishwa vikali kwa kitendo hicho.”
Katika mkutano na waandishi wa habari huko Japan, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema “ Tunahuzunishwa sana na vifo vya watu. Kila ishara kwa uhakika ni kwamba roketi hiyo ilirushwa na Hezbollah.
Forum