Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 18:21

Mvua kubwa yasababisha vifo vya watu 17 Sudan


Mvua kubwa imesababisha majengo kubomoka na kupelekea vifo vya watu 17 kaskazini mwa Sudan, huku nchi hiyo ikikabiliwa na mapigano ya takriban miezi 16 kati ya vikosi pinzani vya kijeshi, afisa wa afya ameliambia shirika la havari la AFP Jumanne.

“Idadi ya walio athirika imeongezeka hadi kufikia 17,” amesema mfanyakazi katika hospitali ya Abu Hamad, mji mdogo katika jimbo la Mto Nile nchini Sudan, uliopo takriban kilomita 400 kaskazini mwa Khartoum.

Takriban nyumba 11,500 zimebomoka, waziri wa miundombinu wa jimbo hilo Samir Saad aliwaambia waandishi wa habari Jumanne, huku takriban watu 170 wamejeruhiwa.

Kila mwaka ifikapo Agosti, mtiririko wa maji kwenye Mto Nile huambatana na mvua kubwa, na kuharibu nyumba na miundombinu ambapo husababisha athabu kubwa kwa watu ikiwamo maisha, sambamba ya kuzuka kwa magonjwa yanayotokana na maji.

Forum

XS
SM
MD
LG