Hali shambulizi hilo limetokea wakati Mashariki ya Kati ikijiandaa kwa uwezekano wa wimbi jipya la mashambulizi ya Iran na washirika wake kufuatia mauaji ya wiki iliyopita ya maafisa wakuu wa kundi la Hamas na Hezbollah.
Roketi mbili za Katyusha zilirushwa katika kituo cha anga cha al Asad magharibi mwa Iraq, vyanzo viwili vya usalama vya Iraq vimesema.
Chanzo kimoja cha usalama cha Iraq kimesema kuwa roketi hizo zilianguka ndani ya kambi hiyo.
Haijabainika iwapo shambulizi hilo lilihusishwa na vitisho vya Iran kulipiza kisasi kutokana na mauaji hayo. Siku ya Jumatano, Iran ilisema Marekani inawajibika katika mauaji ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh mjini Tehran kwa sababu ya uungaji mkono wake kwa Israel.
Forum