Rais wa Marekani Joe Biden amezindua pendekezo lililosubiriwa kwa muda mrefu la kufanya marekebisho kwenye Mahakama ya Juu ya Marekani.
Baraza la Taifa la uchaguzi la Venezuela limesema Jumatatu kwamba Rais Nicholas Maduro, ameshinda urais kwa muhula mwingine, licha ya upinzani kuamini kuwa ulishinda uchaguzi huo.
Israel Jumapili ilishambulia ngome za Hezbollah nchini Lebanon baada ya shambulizi la roketi kutoka Lebanon kuua watu 12 kwenye uwanja wa mpira katika milima ya Golan.
Maelfu ya waombolezaji Jumapili wamehudhuria mazishi ya watoto 12, na vijana waliouwawa na roketi kwenye eneo la Isreal linalokaliwa la milima ya Golan, wakati Israel ikiapa kujibu vikali kundi la Hezbollah la Lebanon, lililofanya shambulizi hilo.
Kiongozi wa Iran Atatollah Ali Khamenei, Jumapili amemuidhinisha Masoud Pezeshkian, kuwa rais wa taifa hilo, ikiwa nafasi kwa mwanasiasa huyo wa mageuzi ambaye pia ni daktari wa upasuaji wa moyo, ya kufufua uchumi ulioathiriwa na vikwazo kutokana na program ya nyuklia.
Treni 7 kati ya 10 za mwendo kasi za Ufaransa Jumamosi zimeanza tena safari zake, siku moja baada ya wahuni kuvuruga mfumo wa usafiri, wakati wa ufunguzi wa michezo ya Olimpiki mjini Paris.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken muda mfupi kabla ya kukutana na mwenzake wa China, Jumamosi, ameomba mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia yajikite katika kukabiliana na changamoto zilizopo, ikiwemo uchokozi na utovu wa sheria wa Beijing kwenye bahari ya South China Sea.
Mashirika ya haki za binadamu yanashutumu mamlaka ya Ufaransa kwa ukandamizaji wa kijamii kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Paris kwa kuwaondoa wahamiaji, wafanyabiashara ya ngono na wengine kuzunguka mji mkuu.
Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatano amekutana na mwenzake wa Syria Bashar al Assad, huko Kremlin, kulingana na video iliyotolewa na Kremlin Alhamisi.
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa ya Asia Kusini Mashariki, pamoja na wanadiplomasia wa juu kutoka washirika muhimu ikiwemo Marekani na China wanakutana kwenye mji mkuu wa Laos, Alhamisi, kwenye kikao cha ASEAN.
Uamuzi wa Rais Joe Biden siku ya Jumapili kujiondoa katika kuwania tena urais ulikuwa ni wa kushangaza huko White House na nje ya hapo, na kuacha hali ya kutokuwa na uhakika kuhusu uteuzi wa Democrati kufuatia hatua hiyo.
Rais Joe Biden ametoa taarifa Jumapili kwamba anajiondoa katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2024.
Kamala Harris, mwanamke wa kwanza kuwahi kuwa makamu rais huenda akateuliwa kushika wadhifa wa juu kwa chama cha Democratic kuwania urais wa Marekani.
Rais wa Marekani Joe Biden Jumapili alitangaza anaondoka kwenye kinyang'anyiro cha urais na kusitisha kampeni yake ya kutaka kuchaguliwa kwa muhula wa pili.
Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskyy Jumapili amesema kuwa Ukraine inahitaji silaha za masafa marefu, ili kulinda miji pamoja na wanajeshi wake dhidi ya droni na makombora ya Russia.
Iran imekemea vikali shambulizi la majibizano la Israel dhidi ya mji wa Hodeida unayomilikiwa na wa Houthi nchini Yemen, ambapo watu 6 wameripotiwa kufa, huku darzeni wengine wakijeruhiwa.
Mahakama ya Bangladesh Jumapili imeondoa sheria yenye utata kwenye mfumo wa utaoji ajira za serikali, ukiwa ushindi kwa wanafunzi baada ya siku kadhaa za maandamano ya kitaifa, ambapo watu kadhaa waliuwawa kwenye makabiliano na polisi.
Mashirika ya ndege, benki, vituo vya televisheni na biashara nyingine duniani kote zilikuwa zikijitahidi kukabiliana na mojawapo ya matatizo makubwa zaidi ya kimtandao katika miaka ya hivi karibuni leo Ijumaa, ambayo yanaonekana kusababishwa na jaribio la kuimarisha programu ya kuzuia virusi.
Viongozi wa Ulaya walifungua mkutano nchini Uingereza wakitoa wito wa kuwepo umoja katika uungaji mkono wao kwa Ukraine katika vita dhidi ya Russia, huku Rais wa Ukraine akimlaumu waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban kwa mkutano wake na Rais wa Russia Vladimir Putin mjini Moscow mapema mwezi huu.
Maafisa wa afya wa Palestina wamesema mashambulizi ya anga ya Israel yaliua watu tisa Jumatano katikati mwa Ukanda wa Gaza.
Pandisha zaidi