Wakati wa hafla ya kumuidhinisha, Ayatollah Ali Khamenei, ameomba Pezeshkian, kuweka kipaumbele chake kwenye nchi jirani, mataifa ya kiafrika na Asia, pamoja na yale yaliounga mkono Iran, na kusaidia kwenye sera ya kigeni za Tehran.
Khamenei amekashifu mataifa ya Ulaya kwa “tabia mbaya dhidi yao,” kutokana na kuweka vikwazo, kuzuia uuzaji wa mafuta na kutuhumu Iran kwa ukiukwaji wa haki za binadamu. Kiongozi huyo pia amekemea Israel kutokana na matendo yake huko Gaza, ya mauaji ya watoto na wanawake, pamoja na watu waliolazwa hospitalini, bila kurusha hata risasi moja dhidi ya vikosi vya Israel.
Wakati wa hafla hiyo, Pezeshkian alikumbuka Jenerali Qassem Soleimani, mratibu wa shughuli za jeshi la Iran, alieuwawa kwenye shambulizi la droni ya Marekani 2020. Pia ameahidi kuzingatia sera dhabiti za kigeni, utawala wa sheria, nafasi sawa kwa watu wa Iran, pamoja na kulinda mazingira.
Forum