Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 03:44

Putin na Assad wakutana Kremlin kuzungumzia hali ya usalama Mashariki mwa Kati


Picha ya Rais wa Syria Bashar al Assad ( kushoto) na Rais wa Russia Vladimir Putin mjini Moscow. Julai 25. 2024
Picha ya Rais wa Syria Bashar al Assad ( kushoto) na Rais wa Russia Vladimir Putin mjini Moscow. Julai 25. 2024

Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatano amekutana na mwenzake wa Syria Bashar al Assad, huko Kremlin, kulingana na video iliyotolewa na Kremlin  Alhamisi.

Putin alimueleza Assad kuwa ana wasi wasi kuhusu kuongezeka kwa mzozo Mashariki ya Kati, bila kutoa taarifa zaidi za mazungumzo yao. Russia imekuwa ikifanya kampeni ya kijeshi nchini Syria tangu 2015, wakati ikishirikiana na Iran, ili kusaidia serikali ya Assad kukabiliana na makundi ya upinzani yenye silaha, na kuchukua tena udhibiti wa sehemu kubwa ya taifa hilo.

Ingawa kwa sasa rasilimali nyingi za kijeshi za Russia zinaelekezwa kwenye vita vya Ukraine, bado inaendelea kuwepo na wanajeshi wake nchini Syria. “Natamani sana kujua maoni yako kuhusu hali inavyoendelea Mashariki ya Kati kwa ujumla,” Putin alimueleza Assad. “Kwa bahati mbaya inaonekana kuna ongezeko la ghasia, na hilo linafanyika Syria pia,” ameongeza kusema.

Putin na Assad walikutana mara ya mwisho Machi 2023, huko Kremlin, wakati wa maadhimisho ya mwaka wa 12 tangu kuzuka kwa vita vya wenye kwa wenyewe. Wakati wa kikao hicho, Putin alisisitiza kuhusu jukumu la jeshi lake katika kurejesha uthabiti wa Syria. Kremlin haijatoa taarifa za kina kuhusu mazungumzo ya viongozi hao, lakini moja ya masuala lilikuwa kuhusu Russia na Uturuki kurejesha uhusiano wa kidiplomasia.

Forum

XS
SM
MD
LG