Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 20:41

Iran yakemea shambulizi la Israel nchini Yemen


Moto waonekana kwenye mji wa Hodieda, Yemen, kufuatia shambulizi la Israel la Jumamosi. Julai 20. 2024.
Moto waonekana kwenye mji wa Hodieda, Yemen, kufuatia shambulizi la Israel la Jumamosi. Julai 20. 2024.

Iran imekemea vikali shambulizi la majibizano la Israel dhidi ya mji wa Hodeida unayomilikiwa na wa Houthi nchini Yemen, ambapo watu 6 wameripotiwa kufa, huku darzeni wengine wakijeruhiwa.

Jumamosi jioni msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Nassar Karani, alikemea tukio hilo vikali, akisema kuwa linaonyesha tabia ya kichokozi ya utawala wa Israel, inaopenda kuuwa watoto. Ndege za kijeshi za Israel Jumamosi zilishambulia bandari hiyo muhimu ya Hodeida, kujibu mashambulizi yaliofanywa na kundi hilo la waasi linaloungwa mkono na Iran.

Shambilizi hilo la Israel, lilikuwa jibu kutokana na shambulizi la droni na Houthi kwenye mji wa Tel Aviv ni la kwanza la moja kwa moja dhidi ya kundi hilo, tangu kuzuka kwa vita vya Gaza miezi 9 iliopita.

Kuzuka kwa ghasia kati ya Israel na mataifa yalio mbali ya kigeni kunatia wasi wasi wa kusambaa kieneo kwa vita vya Gaza. Israel Jumamosi jioni imedhibitisha kufanya mashambulizi ya Hodeida kwa kutumia ndege za kijeshi zilizotengenezewa Marekani za F-15 NA F-35, ili kujibu mamia ya mashambulizi huto kwa Houthi.

Israel, Marekani, Uingereza pamoja na washirika wengine wa magharibi wamenasa karibu droni zote zilizorushwa ma wa Houthi.Hata hivyo Ijumaa iliopita, droni moja kutoka kwa wa Houthi ilipenya kwenye mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel na kuanguka mjini Tel Aviv, na kuuwa mtu mmoja.

Forum

XS
SM
MD
LG