Mashambulizi ya anga ya Israel yaliua watu 60 katika maeneo ya kusini na katikati mwa Gaza, kulingana na maafisa wa afya katika eneo la Palestina, huku Israel ikitaka kuwatokomeza wanamgambo wa Hamas ambao inawatuhumu kujificha katika maeneo yanayokaliwa na watu wengi.
Maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamethibitishwa kwamba kundi la wanamgambo magharibi mwa nchi hiyo, liliwaua wanajeshi tisa katika kambi ya jeshi katika kijiji kimoja mwishoni mwa wiki.
Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani Jumatatu amesema jaribio la mauaji dhidi ya rais wa zamani Donald Trump wakati wa mkutano wa kampeni yake mwishoni mwa Juma lilionyesha “uzembe “ katika usalama ambao hauwezi kukubalika kutokea tena.
Vyombo mbalimbali vya usalama vimeharakisha kutafuta majibu siku ya Jumapili, kabla ya siku moja baada ya aliyetaka kuwa muuaji kumfikia karibu na kupiga risasi na kumjeruhi rais wa zamani Donald Trump katika mkutano wa hadhara katika vijiji vya jimbo la Pennsylvania.
Idara ya upelelezi ya Marekani, FBI, ilisema Jumapili kuwa imemtambulisha Mathew Crooks mwenye umri wa miaka 20 kama aliyehusika kwenye jaribio la mauaji la Jumamosi la aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Dada mwenye nguvu wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, Kim Yo Jong, Jumapili ameapa kujibu kampeni mpya ya Korea Kusini ya kuandika mabango dhidi ya Korea Kaskazini, ikiashiria kuwa taifa hilo huenda likaanza tena kurusha puto zenye takataka ndani ya Korea Kusini.
Kampuni inayomiliki haki za kuokoa meli ya Titanic inaanza safari yake ya kwanza , hilo likifanyika mwaka mmoja baada ya mkasa wa chombo kilichokuwa kimebeba watu kutoka kwa kampuni nyingine kuuwa watu watano.
“Rais Trump analishukuru jeshi la polisi na watoa huduma za dharura waliomfikia haraka baada ya tukio hili la kinyama,” alisema msemaji wake Steven Cheung katika taarifa yake. “Anaendelea vizuri na anafanyiwa uchunguzi katika hospitali ya eneo hilo.”
Rais wa Marekani Joe Biden amekataa wito wa baadhi ya viongozi wa chama chake cha siasa kuachia azma yake ya kugombea kufuatia mdahalo na Donald Trump mwezi uliopita ambapo Biden mara nyingine alipata shida kujieleza.
Jeshi la Israel Alhamisi limefanya mashambulizi kwenye mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah, wakilenga kile walichosema ni wanamgambo waliorusha roketi kutoka mji huo.
Waziri mkuu wa India, Narendra Modi Jumatano wakati akiwa kwenye ziara ya Austria amesema kuwa nchi yake inaunga mkono juhudi za kuleta amani Ukraine.
Shirika la habari la serikali ya China, Xinhua limesema kuwa watu sita wamekufa kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kusini magharibi mwa China, wakati hali ya joto kali kuliko kawaida ikishuhudiwa kwenye msimu huu wa joto.
Takriban watu 25 wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya shambulizi la anga Jumanne kwenye shule iliyogeuzwa makazi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao, kwa mujibu wa maafisa wa afya wa Palestina.
Mataifa wanachama wa NATO Jumanne wanaanza mkutano wao mjini Washington DC, ajenda kuu ikiwa ni uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine.
Kuongezeka kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Russia na Korea Kaskazini kumepelekea umuhimu wa Japan wa kuimarisha ushirikiano wake na muungano wa NATO, wakati tishio la kieneo limekuwa likiongezeka, waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida, ameliambia shirika la habari la Reuters.
Waziri mkuu wa India Narendra Modi anaelekea Russia Jumatatu kwa ziara ya siku mbili, ili kuimarisha ushirikiano, wakati Moscow ikiwa na uhusiano wa karibu sana na China ambayo ni hasimu mkubwa wa India.
Maafisa wawili kutoka kundi la wanamgambo la kiislamu la Hamas wamesema Jumapili kwamba wanasubiri majibu kutoka Israel kuhusu pendekezo lao la sitisho la mapigano, siku 5 baada ya kukubali sehemu muhimu ya mpango wa Marekani, unaolenga kumaliza vita vya Gaza, vilivyodumu kwa miezi 9 sasa
Wapiga kura wa Tokyo Jumapili wamepiga kura zao ili kuamua kama wamchague tena mconservative Yuriko Koike, kama gavana wa mji huo mkuu wa Japan, kwa muhula wa tatu wa miaka minne.
Afrika haikuvutia sana uwekezaji wa kigeni mwaka jana na makubaliano ya kifedha yalishuka kwa asilimia 50 mpaka dola bilioni 64, kwa mujibu wa ripoti mpya.
Marekani imepongeza usitishwaji wa muda wa wiki mbili kwa mapigano mashariki mwa DRC, kwa sababu za kibinadamu, White House imesema. Mapigano makali yamekuwa yakiendelea kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa kundi la M23, wanaoungwa mkono na Rwanda.
Pandisha zaidi