Tangu mwishoni mwa Mei, Korea Kaskazini imerusha puto nyingi zikiwa zimebeba taka za aina tofauti pamoja na mbolea kuelekea Korea Kusini, hilo likifanyika nyakati za usiku, dada yake Kim akisema kuwa yalikuwa majibu dhidi ya wanaharakati wa Korea Kaskazini kurusha vijikaratasi vyenye maneno ya kisiasa dhidi ya Kaskazini.
Kufikia sasa hakuna taka zenye sumu zilizorushwa. Korea Kusini ilijibu kwa kusitisha makubaliano ya 2018 ya kupunguza taharuki na Korea Kaskazini, wakati ikirejea tena mazoezi ya silaha za moto kwenye mpaka. Kupitia taarifa iliotolewa kupitia vyombo vya habari vya serikali.
Kim Yo Jong amesema kuwa majikaratasi yenye matusi kutoka Korea Kusini yamepatikana tena kwenye mpaka na kwenye baadhi ya maeneo ndani ya Korea Kaskazini. Ameongeza kusema kuwa licha ya maonyo kutoka Kaskazini, Korea Kusini inaendelea na mchezo huo mbaya.
Forum