Kimbunga Beryl kilitua kwenye Peninsula ya Yucatan ya Mexico karibu na mji wa mapumziko wa Tulum kama dhoruba ya kiwango cha pili mapema Ijumaa, kikifagia miti na kusababisha kukatika kwa umeme, baada ya kusababisha uharibifu, na vifo vya takriban watu 11 kote Karibean.
Uingereza ina Waziri mkuu mpya. Keir Starmer anakuwa Waziri mkuu wa 58 wa taifa hilo, ambapo chama chake cha Leba kinarejea tena mamlakani baada ya zaidi ya mwongo mmoja kama upinzani, kufuatia ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi nchini humo.
Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Volker Turk, ameonya kuwa uchaguzi ujao wa rais nchini Venezuela, huenda usiwe huru na wa haki kutokana na ukandamizaji uliotanda kote nchini, ukizuia sauti za wananchi kusikika.
Kuvuja kwa kemikali mapema Alhamisi, kwenye kitengo cha uhandisi cha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur, Malaysia, kumesababisha takriban watu 20 kuumwa, afisa wa huduma ya dharura amesema.
Wapiga kura wa Uingereza leo Alhamisi wameshiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao kwa kiasi kikubwa unatarajiwa kutoa ushindi kwa chama cha upinzani cha Labour, na kumaliza utawala wa karibu muongo mmoja na nusu wa utawala wa chama cha Conservative.
Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano ameapa kuendelea kuwania muhula wa pili, akipuuza hisia zinazozidi kuongezeka kwamba kushindwa kufanya vizuri katika mdahalo wa kwanza, kutasababisha ajiondowe kwenye kampeni kuelekea uchaguzi wa tarehe 5 Novemba.
Waendesha mashtaka wa Ufaransa wameiomba Mahakama ya juu nchini humo kuamua kuhusu uhalali wa hati ya kimataifa ya kumkamata Rais wa Syria Bashar al-Assad.
Israel ilitoa Amri ya kuwahamisha Wapalestina katika baadhi ya maeneo ya Khan Younis na maeneo jirani, amri ambayo huenda inaashiria Israel inapanga kuushambulia tena mji huo wa kusini mwa Gaza.
Mahakama ya Juu ya Marekani leo Jumatatu imetoa maamuzi kuwa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ana kinga kwa matendo yoyote rasmi aliyofanya ya kujaribu kubadili kuchaguliwa kwake tena katika uchaguzi wa mwaka 2020, lakini hana kinga kwa matendo yasiyo rasmi.
Umoja wa Ulaya imeishutumu Mmiliki wa Facebook, Meta Jumatatu kwa kukiuka kanuni za kidigitali ya jumuiya hiyo, ikifungua njia ya uwezekano wa kupigwa faini ya mabilioni ya euro.
Hungary Jumatatu inachukua uongozi wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya, wakati ikiahidi kuongoza kwa uadilifu, licha ya wasi wasi mwingi kutokana na kile wakosoaji wanachokiona kuwa utawala wa kiimla, na urafiki wao mkubwa na serikali ya Russia.
Marekani inaendelea kusukuma mpango wa amani kati ya Israel na Hamas unawahusisha wapatanishi wa kikanda Misri na Qatar. Wakati huo huo, wote Israel na Hamas wanasema hakuna maendeleo wakati mapigano yameongezeka huko Gaza.
Kimbunga kilichopewa jina Beryl kilikuwa kinakaribia kusini mashariki mwa Caribbean, wakati maafisa wa serikali wakiwasihi wakazi Jumapili jioni, kuchukua hifadhi ili kuepuka hatari zake, kilitarajiwa kuwa kwenye kiwango hatari cha tatu.
Wapiga kura wa Ufaransa wamekipa ushindi chama cha mrengo mkali wa kulia cha National Rally katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge Jumapili na kuiweka nchi katika hali isiyo na uhakika, kulingana na makadirio ya matokeo ya uchaguzi.
Polisi wa Switzerland wamesema leo Jumapili kwamba watu wawili wamekufa, huku mwingine akitoweka, kufuatia mvua kubwa zilizosababisha maporomoko ya ardhi, kusini mashariki mwa taifa hilo.
Wapiga kura wa Ufaransa leo Jumapili wameanza kupiga kura, ikiwa duru ya kwanza ya uchaguzi maalum wa bunge, ambao huenda ukaweka serikali kwenye mikono ya vyama vyenye msimamo mkali wa kulia, kwa mara ya kwanza tangu enzi ya Nazi.
Polisi wa Switzerland wamesema Jumapili kwamba watu wawili wamekufa, huku mwingine akitoweka, kufuatia mvua kubwa zilizosababisha maporomoko ya ardhi, kusini mashariki mwa taifa hilo.
Shambulizi la ndege isiyo na rubani za Ukraine lililolenga nyumba moja katika kijiji kilicho kwenye mpaka na Russia liliua watu watano, wakiwemo watoto wawili, gavana wa eneo hilo alisema Jumamosi.
Raia wa Mauritania walipiga kura siku ya Jumamosi katika uchaguzi wa rais ambao kiongozi wa sasa wa nchi hiyo, Mohamed Ould Ghazouani, anatarajiwa kushinda.
Iran itafanya duru ya pili ya uchaguzi wa rais ili kuamua ni nani atachukua nafasi ya rais wa zamani marehemu Ebrahim Raisi, afisa mmoja alisema Jumamosi, baada ya duru ya kwanza ya zoezi hilo, lililofanyika Ijumaa, kutobaini mshindi wa moja kwa moja.
Pandisha zaidi