Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 17:28

EU yamshutumu mmiliki wa Facebook kwa kukiuka kanuni za kidigitali 


FILE - Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Meta Mark Zuckerberg
FILE - Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Meta Mark Zuckerberg

Umoja wa Ulaya imeishutumu  Mmiliki wa Facebook, Meta Jumatatu kwa kukiuka kanuni za kidigitali ya jumuiya hiyo, ikifungua njia ya uwezekano wa kupigwa faini ya mabilioni ya euro.

Tuhuma hizo dhidi ya kampuni hiyo ya kubwa ya teknolojia ya Marekani inafuatia wiki iliyopita kugundulika makosa dhidi ya Apple ikiwa ni mara ya kwanza Brussels kutoa tuhuma rasmi chini ya Sheria ya Masoko ya Kidigitali ya EU (DMA).

Kesi hii ya hivi sasa inaangazia juu ya muundo wa usajili wa matangazo ya bure mapya ya Meta kwa ajili ya Facebook na Instagram, ambao umeibua malalamiko kadhaa kuhusu wasiwasi wa faragha ya watumiaji mitandao.

Meta-Attorneys General-Letter
Meta-Attorneys General-Letter

Mfumo wa “Malipo au idhini” wa Meta unamaanisha kuwa watumiaji wanatakiwa kulipia kuepuka takwimu kukusanywa, au wakubali kutoa takwimu zao kutumiwa na Facebook na Instagram ili waweze kutumia mitandao hiyo bure.

Umoja wa Ulaya ilisema imeitaarifu Meta kuhusu “maoni yake ya awali” kuwa muundo huo uliozinduliwa na kampuni hiyo mwaka jana “unakinzana” na DMA.

Forum

XS
SM
MD
LG