Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant, Jumapili ametembelea Washington, ili kuzungumzia kuhusu awamu nyingine ya vita vya Gaza, pamoja na ghasia zinazoendelea kwenye mpaka wa Israel na Lebanon, ambako makabiliano na wapiganaji wa Hezbollah, yamezua wasi wasi wa kuongozeka kwa ghasia hizo.