Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 04:51

Putin na Kim Jong Un wasaini mkataba wa ushirikiano


Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa na mwenyeji wake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, mjini Pyongyang. Jumatano Juni 19, 2024.
Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa na mwenyeji wake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, mjini Pyongyang. Jumatano Juni 19, 2024.

Rais wa Russia Vladmir Putin na mwenyeji wake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un wametia saini makubaliano mapya ya ushirikiano Jumatano, yanayojumuisha ahadi ya msaada wa pamoja kama nchi zao zitavamiwa, wakati wote wanakabiliwa na mizozo inayoongozeka na nchi za magharibi.

Hii inaashiria kuimarishwa kwa ushusiano wa karibu baina ya Moscow na Pyongyang tangu Jamhuri ya Russia ilipovunjika mwaka 1991.

Putin alitembelea Korea Kaskazini kwa mara ya kwanza baada ya miaka 24 wakati Marekani na washirika wake zikieleza kuendelea kuwa na wasiwasi kuhusu mpango wa silaha ambao nchi hiyo inaipa Moscow kwa ajili ya kujihami katika vita vyake na Ukraine.

Kwa upande wake Pyongyang itaweze kupata msaada wa kiuchumi na teknolojia ambao utaweza kuzidisha tishio la sialaha za nyuklia za utawala wa Kim na program yake ya makombora.

Maelezo ya ushirikiano huo haukuwekwa bayana, lakini viongozi wote wawili wamesema kwamba ni kuimarisha kwa kiwango cha juu ushirikiano wao.

“Kuhusiana na hili shirikisho la Russia haliondowi uwezekano wa kujenga ushirikiano wa kijeshi na kiufundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea kwa mujibu wa nyaraka iliyosainiwa leo.” Putin.

Rais wa Russian Vladimir Putin na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
Rais wa Russian Vladimir Putin na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Naye kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, alisema kuwa “sina shaka kwamba mkataba huu wenye nguvu uliotiwa saini baina ya nchi zetu mbili utakuwa wenye tija, mafanikio na hasa ni wa kupenda amani na ulinzi, "

Na kuongeza kuwa mkataba huo " wenye lengo la kukuza na kutetea maslahi ya kimsingi ya watu wa nchi hizi mbili ambao utakuwa na nguvu mpya ya kimataifa usio na utawala, ukangamizaji, ubabe na mamlaka ya upande mmoja."

Wakati wa sherehe hizo zilizofanyika katika bustani ya Kim II Sung, wakazi wa Korea Kaskazini wakiwa wamevalia mavazi yenye rangi za kitaifa nyekundu, nyeupe na shati za blue walipeperusha mashada ya maua, huku bendi ya kijeshi ikicheza nyimbo za kizalendo.

Viongozi hao pia walikagua gwaride la heshima kabla ya kuondoka ili kufanya mashauriano ambayo yalijumuisha mazungumzo ya saa mbili ya moja kwa moja kulingana na vyombo vya habari vya Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG