Timu ya makamanda wa polisi kutoka Haiti, Jumanne wamekutana na mkuu wa polisi wa Kenya, jijini Nairobi, kabla ya upelekaji wa polisi wa Kenya kwenye taifa hilo la Caribbean lililokumbwa na ghasia, hatua inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni
Baraza la Senate la Thailand Jumanne limepiga kura kwa wingi kuidhinisha mswada utakao halalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja, ikiwa hatua ya mwisho kuelekea taifa hilo kuwa la kwanza Mashariki mwa Asia kupitisha sheria hiyo.
Takriban wagonjwa tisa wamekufa mapema Jumanne, baada moto kuzuka kwenye hospitali iliyopo kwenye mji wa kaskazini mwa Iran, wa Rasht, chombo cha habari cha serikali kimeripoti.
Korea Kusini imesema Jumanne kuwa darzeni ya wanajeshi wa Korea Kaskazini wamevuka mpaka wenye ulinzi mkali, lakini wakarejea baada ya risasi za onyo kupigwa.
Wanamgambo wa Al-Shabab wamedhoofisha mafanikio yote ambayo jeshi la taifa la Somalia liliyapata katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, na sasa wanashirikiana na kundi la wanamgambo wa Houthi kuimarisha nguvu zao, kulingana na maafisa wakuu wa wizara ya ulinzi ya Marekani.
Rais wa Russia Vladimir Putin anatarajiwa kuwasili mjini Pyongyang leo Jumanne katika ziara nadra ambayo inaweza kupelekea kusainiwa “mkataba wa ushirikiano wa kimkakati,” kulingana na maafisa wa Kremlin.
Mratibu wa mawasiliano ya kimkakati wa Baraza la Kitaifa la Usalama nchini Marekani (NSC), John Kirby, Jumatatu alitetea uamuzi wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuvunja baraza la mawaziri la vita, na kusema kwamba hayo ni maamuzi ya ndani.
Mwanajeshi wa Marekani Gordon Black Jumatatu amekana mashitaka kwenye ya mahakama ya Russia, kwa shutuma za kutishia kumuuwa mpenzi wake wa kike, lakini alikiri kumuibia fedha ,kulingana na chombo cha habari cha serikali ya Russia.
Mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis Jumapili ametoa wito wa kusitishwa kwa ghasia na mauaji ya raia kwenye jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo.
Umati mkubwa wa mahujaji Jumapili umefanya ibada ya kumpiga vijiwe shetani nchini Saudi Arabia huku joto likiwa kali sana. Hatua hii inaadhimisha siku ya mwisho ya Hijaa kwa waislamu, na mwanzo wa sherehe za Eid Al Hajj kwa waislamu kote duniani.
Serikali ya Taliban ya Afghanistan imesema Jumapili kwamba tatuma ujumbe wake kwenye kongamano la Umoja wa Mataifa la siku mbili kuhusu Afghanistan, lililopangwa Juni 30 mjini Doha, Qatar.
Thailand imewasilisha ombi lake la kujiunga na muungano wa mataifa yanayoendelea wa BRICS, unaojumuisha Brazil, Russia, India na Afrika Kusini, ingawa wataalam wanaeleza kuwa na wasi wasi wa iwapo hatua hiyo inafaa.
Jeshi la Sudan limesema Ijumaa kwamba limemuua Ali Yagoub Gibril, kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la kijeshi la Rapid Support Forces, RSF, ambaye alikuwa amekewa vikwazo na Marekani, wakati wa mapigano kwenye mji uliozingirwa wa al-Fashir kaskazini mwa Darfur.
Rais wa Russia Vladimir Putin Ijumaa ameahidi kuamuru sitisho la haraka la mapigano nchini Ukraine na kuanza mashauriano, iwapo Kyiv itaanza kuondoa wanajeshi wake kutoka kwenye mikoa minne iliyochukuliwa na Moscow 2022, na kusitisha mpango wa kujiunga na NATO.
Mahakama ya Israel Ijumaa imethibitisha, na kuongeza muda wa siku 35 kwa serikali kufunga kituo cha televisheni cha Al Jazeera, chenye makao yake Qatar, wizara ya sheria imesema .
Mgombea urais wa Marekani Donald Trump amerejea kwenye kampeni baada ya kukutwa na hatia huko New York kwa kugushi rekodi za biashara.
Donald Trump amerejea kwenye kampeni ya kisiasa wiki hii akiwa rais wa kwanza wa Marekani kukutwa na hatia ya uhalifu wakati ambapo ni mgombea mkuu wa chama.
Uchumi wa Marekani ni moja ya masuala makubwa sana kwa wapiga kura katika kinyang’anyiro cha urais mwaka huu kati ya Joe Biden and Donald Trump.
Msemaji wa jeshi la Congo amesema Jumapili kwamba idadi ya vifo kutokana na shambulizi la Ujumaa imefikia 41.
Pandisha zaidi