Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 21, 2025 Local time: 09:13

Idadi ya vifo vya kutokana na shambulizi la DRC yafikia 41


Wakazi wa Goma Mashariki mwa Congo wakiandamana kupinga mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa waasi. Picha ya maktaba.
Wakazi wa Goma Mashariki mwa Congo wakiandamana kupinga mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa waasi. Picha ya maktaba.

Msemaji wa jeshi la Congo amesema  Jumapili kwamba idadi ya vifo kutokana na shambulizi la Ujumaa imefikia 41.

Liuteni Kanali Mak Hazujay, amesema kuwa shambulio hilo lilitekelezwa na waasi wa kundi la Allied Democratic Forces, ADF, kwenye jimbo la Mashariki la Kivu Kaskazini. ADF ambalo ni tiifu kwa kundi la kigaidi la Islamic State, lenye makao yake mashariki mwa Congo limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara, kwenye eneo hilo lenye makundi mengi ya wanamgambo.

Kundi hilo lililoanzishwa Uganda pia linalaumiwa kutokana na shambulizi jingine la mapema wiki hii ambalo liliuwa takriban watu 16. Afisa mmoja wa kieneo ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki na mapanga walifanya shambulizi la usiku kucha Ijumaa, kwenye vijiji karibu na mji wa Beni.

Visindi Nick Junior ambaye ni kiongozi wa asasi ya kiraia katika eneo hilo amesema kuwa kituo cha afya kilichomwa moto wakati watu 6 walijeruhiwa kando na wale 41 waliouwawa. Kufikia sasa serikali haijasema lolote kufuatia shambulizi hilo, na msemaji wa serikali hakujibu maombi ya shirika la habari la Reuters ikimtaka atoe maoni.

Forum

XS
SM
MD
LG