Kurusha vijiwe na miongoni mwa hatua za mwisho za Hijja, ambayo ni moja ya nguzo tano za kiislamu. Imekuja siku moja baada ya mahujaji takriban milioni 1.8 kukusanyika katika mlima mtakatifu, unaojulika kama Mlima Arafat, nje kidogo ya mji mtakatifu wa Makka, ambako mahujaji wa kiislamu wanakwenda kufanya ibada ya siku tano ya hijja.
Mahujaji waliondoka Mlima Arafat Jumamosi jioni na kwenda kukaa karibu na eneo linalojulikana kama MUZDALIFA, ambako walikusanya vijiwe na kuvitumia katika kumpiga shetani.
Nguzo za kurusha vijiwe ziko katika sehemu nyingine takatifu huko Makka, kunakoitwa Minna, ambako Waislamu wanaamini imani ya Nabii Ibrahim ilijaribiwa wakati Mwenyenzi Mungu alipomuamuru kumtoa mtoto wake wa pekee wa kiume Ismail. Ibrahim alikuwa tayari kutimiza amri ya Mwenyenzi Mungu, lakini Mungu alizuia hilo lisifanyike.
Forum