Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 14:07

Saudi Arabia imemteua balozi wake wa kwanza nchini Syria tangu 2012


Ramani ya Saudi Arabia na nchi zilizo jirani nao.
Ramani ya Saudi Arabia na nchi zilizo jirani nao.

Syria ilisimamishwa uanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwa zaidi ya muongo mmoja

Saudi Arabia imetangaza uteuzi wa balozi wake wa kwanza nchini Syria tangu kusitisha uhusiano wake na Damascus katika kipindi cha miaka 12, ikiashiria kulegeza uhusiano tangu nchi hiyo iliyokumbwa na vita ilipojiunga tena na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

Uteuzi wa Faisal al-Mujfel kama balozi wa kwanza wa Saudi Arabia nchini Syria tangu mwaka 2012 ulitangazwa na shirika la habari la Saudi Arabia. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu Syria ikubaliwe tena katika jumuiya ya nchi 22 wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

Syria ilisimamishwa uanachama kwenye kundi hilo kwa zaidi ya muongo mmoja, kutokana na ukandamizaji wa kikatili unaofanywa na Rais Bashar al-Assad dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali mwaka 2011. Riyadh ilivunja uhusiano wake na Damascus mwaka 2012. Vyombo vya habari vya serikali ya Syria na mamlaka hazikutoa tamko lolote kuhusu maendeleo hayo.

Ghasia zilizogeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, ambavyo sasa viko katika mwaka wake wa 14, vimesababisha vifo vya takribani watu nusu milioni na kuwakosesha makazi nusu ya watu milioni 23 wa nchi hiyo. Kwa muda mrefu imeendelea kutengwa kwa kiasi kikubwa, na hivyo imefanya juhudi za kutafuta suluhisho la kisiasa la kumaliza hali hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG