Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 17, 2025 Local time: 15:54

Utawala wa Taliban wa Afghanistan kutuma wajumbe wake kwenye mazungumzo ya Qatar


Wajumbwa wa utwala wa Taliban wa Afghanistan wakihudhuria mazungumzo ya Doha, Qatar, Nov. 21, 2020.
Wajumbwa wa utwala wa Taliban wa Afghanistan wakihudhuria mazungumzo ya Doha, Qatar, Nov. 21, 2020.

Serikali ya Taliban ya Afghanistan imesema Jumapili kwamba tatuma ujumbe wake kwenye kongamano la Umoja wa Mataifa la siku mbili kuhusu Afghanistan, lililopangwa Juni 30 mjini Doha, Qatar.

Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa viongozi wa Afghanistan kuhudhuria kikao cha wajumbe wa kimataifa kuhusu taifa lao, tangu katibu mkuu wa UN Antonio Guterres alipoanza mchakato huo mwaka mmoja uliopita, kwa lengo la kuimarisha namna jumuia ya kimataifa inavyotangamana na Taliban.

Zabihullah Mujahid ambaye ni msemaji mkuu wa Taliban ameambia televisheni ya kitaifa mapema Jumapili, kwamba serikali yao ilifanya mashauriano ya ndani kuhusu ajenda kwenye mkutano wa Doha ambao unafanyika kwa mwaka wa tatu, huku wakikubaliana kushiriki.

Alitetea uamuzi huo bila kutoa masharti yoyote kutoka kwa serikali yake, akisema kuwa kila mkutano unaolenga kuwezesha upelekaji wa misaada ya kibinadanu pamoja na uwekezaji ndani ya Afganistan ni muhimu.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa kikao hicho cha 3 cha Doha kinalenga kuimarisha utangamano na Taliban na Afganistan kwa ujumla, kwa njia madhubuti na iliyoratibiwa kwa makini.

Forum

XS
SM
MD
LG