Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 20, 2025 Local time: 22:59

Mafuriko Afghanistan yasababisha vifo vya watu 50

Mafuriko Afghanistan
Mafuriko Afghanistan

Mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua kubwa za msimu magharibi mwa Afghanistan yamesababisha vifo vya takriban watu 50 na wengine kadhaa hawajulikani walipo, afisa wa Taliban alisema Jumamosi, akiongeza kuwa idadi ya waliofariki ilitokana na ripoti za awali na huenda ikaongezeka.

Afghanistan imekuwa ikishuhudia mvua kubwa za msimu zisizo za kawaida.

Jimbo lililoathirika zaidi la Ghor limepata hasara kubwa ya kifedha, alisema Abdul Wahid Hamas, msemaji wa gavana wa jimbo hilo, baada ya maelfu ya nyumba na mali kuharibiwa na mamia ya hekta za ardhi ya kilimo kuharibiwa kufuatia mafuriko ya Ijumaa, ukiwemo mji mkuu wa Feroz Koh.

Msemaji mkuu wa serikali ya Taliban alichapisha kwenye mtandao wa kijamii wa X, akiomboleza "kupoteza Waafghanistan," na akahimiza "mamlaka kutoa msaada wote muhimu ili kupunguza mateso." Pia alitoa wito kwa kusaidia na mashirika ya kibinadamu kutoa misaada kwa jamii zilizoathirika.

Wiki iliyopita, shirika la chakula la Umoja wa Mataifa lilisema mvua kubwa isiyo ya kawaida nchini Afghanistan imesababisha vifo vya zaidi ya watu 300 na kuharibu maelfu ya nyumba, hasa katika mkoa wa kaskazini wa Baghlan, ambao ulikumbwa na mafuriko tarehe 10 mwezi huu.

Forum

XS
SM
MD
LG