Black alikamatwa mwezi uliopita katika mji wa mashariki wa Vladivostok, akiwa mmoja wa darzeni ya wamarekani wanaoshikiliwa Russia wakikabiliwa na mashitaka ya uhaini, wakati kukiwa na mgororo kati ya Moscow na Washington, juu ya vita vya Ukraine.
Chombo cha habari cha RIA kimesema kuwa mwanajeshi huyo ambaye amezungumza kupitia mkalimani, alikiri kumuibia mpenzi wake Alexandra Vashchuk ruble, 10,000 za Russia, ambazo ni sawa na dola 113 za marekani, bila ya kuwa na nia yoyote ya kumdhuru. Katika shitaka la pili Black amekanusha kumkaba na kusababisha kuhofia maisha yake.
Ripoti zimesema kuwa Vashchuck ameiambia mahakama kwamba Black anahitaji msaada wa kisaikolojia na wala siyo adhabu kali, na kwamba hayuko tayari kurudiana naye kwa kuwa hajalipwa fidia. Chombo kingine cha habari cha serikali kimesema kuwa Vashchuk alidai kuwa Black amekuwa akimnyanyasa zaidi ya mara moja hapo nyuma.
Wawili hao wanasemekana kukutana Korea Kusini ambako Black alikuwa ametumwa kikazi. Pentagon imesema kuwa Black alivunja sheria za kijeshi kwa kuingia Russia bila idhini, akipitia China.
Forum