Mazungumzo yao yanalenga kuangazia kuongezeka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Myanmar, na kuongezeka kwa mivutano kwenye bahari ya South China Sea, miongoni mwa masuala mengine ya kikanda.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja pembeni mwa mkutano huo mjini Vientiane, unaofanyika wakati Beijing, na Washington, wakijitahidi kuongeza ushawishi wao kwenye eneo hilo.
Waziri wa mambo ya nje wa Laos, Saleumxay Kommasith amewashukuru wanachama wa ASEAN, pamoja na washirika wao, kwa juhudi zao za pamoja ambazo zimepelekea hatua zilizopigwa, huku akisisitiza umuhimu wa kundi hilo wa kuzingatia amani na uthabiti.
Kwa mataifa wanachama wa ASEAN, Indonesia, Thailand, Singapore, Ufilipino, Vietnam, Malaysia, Myanmar, Cambodia, Brunei na Laos, suala la ghasia za Myanmar ni kipaumbele cha mazungumzo yao.
Forum