White House Alhamisi imesema kwamba mazungumzo ya kusitisha mapigano huko Gaza ambayo yameanza tena huko Doha, nchini Qatar pamoja na maafisa wakuu wa Marekani, “yameanza kwa matumaini” lakini hakuna matumaini ya kufikia makubaliano mara moja.
Sweden Alhamisi iliripoti kisa cha kwanza cha aina ya ugonjwa unaombukiza sana wa mpox ambao kwa sasa unaendelea kusambaa eneo la Afrika ya kati na Afrika mashariki.
Mashirika ya kutetea haki za waandishi wa habari yanasema kusimamishwa kwa leseni za utangazaji, kukamatwa kwa waandishi wa habari na kufungwa kwa vyombo vya habari nchini Afghanistan, inaonyesha kuwa Taliban wanaendelea kukandamiza vyombo vya habari.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy Jumatano alisema wanajeshi wa nchi yake “wanazidi kusonga mbele” ndani ya mkoa wa Russia wa Kursk na kudai kwamba mamia ya wanajeshi wa Russia walitekwa nyara au kujisalimisha.
Shirika la afya duniani WHO lilitangaza katika mkutano wake Jumatano kuwa ugonjwa wa Mpox ni dharura ya kimataifa ya afya ya umma.
Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne alitembelea kituo maarufu cha kutibu Cancer katika jimbo la Lousiana na kutangaza dola milioni 150 katika ufadhili wa utafiti kuelekea lengo la kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya saratani nchini Marekani.
Kundi la Hamas limesema wanajeshi wake walimuua mateka mmoja wa Israel na kujeruhi wengine wawili, huku White House ikionya Jumatatu kwamba shambulizi la Iran dhidi ya Israel linaweza kufanyika muda wowote.
Matarajio ya makubaliano ya kusitisha mapigano kutokana na mazungumzo ya amani nchini Sudan yaliyofadhiliwa na Marekani wiki hii hayapo mezani kwa sasa, kwani pande zinazopigana hazijathibitisha kuhudhuria kwao.
Kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana ulimwenguni kilishuka kwa asilimia 13 mwaka 2023, kikiwa kiwango cha chini kwa kipindi cha miaka 15.
Maafisa wa afya wa Gaza wamesema kuwa Israel, Jumapili imetoa ilani kwa watu ya kuondoka kusini mwa Gaza, baada ya shambulizi dhidi ya shule iliyokuwa imegeuzwa hifadhi upande wa kaskazini kuuwa takriban wapalestina 80.
Kiongozi wa upinzani wa Venezuela, Jumamosi ameomba rais Nicolas Maduro kumaliza ‘ghasia na mateso,’ saa chache baada ya mahakama kusema kuwa uamuzi wake unaotarajiwa kuhusu utata wa uchaguzi wa Julai 28 hauwezi kukatiwa rufaa.
Shirika la Ulinzi wa Jamii la Gaza limesema Jumamosi kwamba idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Israel dhidi ya shule iliyokuwa imetoa hifadhi kwa watu waliokoseshwa makazi, imepita 90, wakati jeshi la Israel likidai kuwa lililenga kituo cha kamandi cha wanamgambo.
Mwanaume aliyefungwa jela kutokana na mauaji ya mwanasiasa wa upinzani wa Russia, Boris Nemtov, ameachiliwa kutoka gerezani baada ya kutia saini mkataba wa kujiunga na opereseheni za kijeshi nchini Ukraine, kulingana na ripoti ya Jumamosi ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali.
Mahakama ya kijeshi mjini Kinshasa, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imewahuku kifo washtakiwa 26 wanaoshutumiwa kuwa wanachama wa kundi la waasi la M23.
Warepublican katika Bunge wanaunga kwa karibu na mgombea urais Donald Trump katika masuala kadhaa muhimu ya sera ya mambo ya nje ikiwa ni pamoja na uungaji mkono wa Marekani kwa Israel.
Wafanyakazi kwenye kiwanda cha kutengeneza manowari cha Australia ,ASC Ltd, Jumatano wameanza mgomo wa siku nne wakidai nyongeza ya mishahara, hatua inayotishia ukarabati wa manowari za zamani, ambazo zinategemewa hadi pale zile zinazotumia nishati ya nyuklia zitakapo wasili katika miaka ya 2030.
Polisi wa Uingereza wanajiandaa kwa maandamano zaidi dhidi ya uislamu Jumatano wakati makundi ya mrengo wa kulia yakiahidi kulenga vituo vya kuomba hifadhi na makampuni ya uhamiaji kote nchini, na kuchochea waandamanaji dhidi ya ufashisti wanaopanga kukabiliana na maandamano.
Marekani imezieleza Iran na Israel kwamba migogoro ya Mashariki ya Kati haipaswi kuongezeka, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken amesema Jumanne, huku kukiwa na hofu kwamba Tehran na washirika wake wanajiandaa kuanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Israeli.
Zaidi ya watu 120 wamekufa kutokana na kiharusi cha joto katika eneo la mji mkuu wa Tokyo, Julai, wakati wastani wa hali ya joto ulipofikia rekodi ya juu na tahadhari ya joto kutolewa katika sehemu kubwa ya mwezi huo, serikali ya Japani imesema Jumanne.
Shirika la anga za juu la Marekani, NASA limechelewesha safari ijayo ya anga ili kutoa muda zaidi katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu kushugulikia chombo cha Boeing kinachosafirisha wanaanga chenye matatizo.
Pandisha zaidi