Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 18:33

120 wafariki dunia kwa sababu ya joto kali Japan


Zaidi ya watu 120 wamekufa kutokana na kiharusi cha joto katika eneo la mji mkuu wa Tokyo, Julai, wakati wastani wa hali ya joto ulipofikia rekodi ya juu na tahadhari ya joto kutolewa katika sehemu kubwa ya mwezi huo, serikali ya Japani imesema Jumanne.

Kwa mujibu wa dakrati mkuu wa Tokyo, wengi kati ya watu 123 waliokufa walikuwa wazee.

Wote isipokuwa wawili walikutwa wakiwa wamekufa ndani ya nyumba, na wengi wao walikuwa hawatumii viyoyozi licha ya kuwa navyo.

Idara za afya za Japani na watabiri wa hali ya hewa mara kwa mara walishauri watu kukaa ndani, kunywa vimiminika vya kutosha ili kuepuka upungufu wa maji mwilini na kutumia kiyoyozi, kwa sababu mara nyingi wazee hufikiri kwamba kiyoyozi si kizuri kwa afya ya mtu na huwa na tabia ya kuepuka kukitumia.

Forum

XS
SM
MD
LG