Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 20:48

Mfungwa wa mauaji wa Russia aachiwa huru kwa sharti la kujiunga kwenye vita vya Ukraine


Picha ya maktaba ya wafungwa wa Russia walioachiliwa kutoka jela ya Ujerumani.
Picha ya maktaba ya wafungwa wa Russia walioachiliwa kutoka jela ya Ujerumani.

Mwanaume aliyefungwa jela kutokana na mauaji ya mwanasiasa wa upinzani wa Russia, Boris Nemtov, ameachiliwa kutoka gerezani baada ya kutia saini mkataba wa kujiunga na opereseheni za kijeshi nchini Ukraine, kulingana na ripoti ya Jumamosi ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali.

Nemtsov aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa rais Vladimir Putin, na pia naibu waziri mkuu wakati wa utawala wa rais Boris Yeltsin, alipigwa risasi na kuuwawa 2015 wakati akivuka daraja moja karibu na Kremlin, mjini Moscow. Mahakama ya Russia 2017 ilitoa hukumu dhidi ya wanaume watano kutokana na mauaji hayo, wakipewa vifungo vya kati ya miaka 11 hadi 20 jela.

Miongoni mwao ni Tamerian Eskerkhanov, ambaye alihukumiwa kama mshirika, na kupewa kifungo cha miaka 14 jela. Machi mwaka huu anesemekana kutia saini mkataba na wizara ya Ulinzi ili kuachiliwa na kujiunga kwenye jeshi.

Maelfu ya wafungwa wa Russia wamejitolea kujiunga kwenye jeshi linalopigana na Ukraine, wakitegemea kuwa huru iwapo watanusurika kwenye uwanja wa vita, kwa mujibu wa msamaha uliotolewa na serikali.

Forum

XS
SM
MD
LG