Washtakiwa 21 kati yao hawakuwepo mahakamani na hawajulikani walipo, walikutwa na makosa ya uhalifu wa kivita, na kupanga njama za kuipindua serikali.
Waasi wa M23, wanaoripotiwa kuungwa mkono na serikali ya Rwanda, wameteka sehemu kadhaa mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo tangu mwishoni mwa mwaka 2021.
Mawakili wa watuhumiwa watano waliokuwa mahakamani wametaka kesi hiyo ifutwe.
Wengine waliohukumia ni viongozi wa ngazi ya juu wa kundi la waasi la M23 akiwemo rais wa kundi hilo Bertand Basimwa, Corneille Nanga, kamanda mkuu Sultani Makenga, wasemaji wa kundi hilo Willy Ngoma na Lawrence Kanyuka.
M23 ni miongozi mwa darzeni ya makundi ya waasi yaliyo mashariki mwa DRC. Idadi kubwa ya makundi hayo yamekuwa yakipigana tangu miaka ya 1990 baada ya kuanguka kwa utawala wa Mobutu Sese Seko.
Mnamo mwezi Machi, serikali ya DRC ilikataa kusikiliza shutuma za mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanayotaka adhabu ya kifo kuondolewa.
Hukumu ya kifo imekuwa ikitumika tangu mwaka 2003, ikiwalenga wanajeshi wanaoshutumiwa kupanga njama za kuipindua serikali.
Me Peter Ngomo - Wakili wa Corneille Nangaa anasema: "Ni jambo la kusikitisha sana. Japo tulidhani hukumu ingekuwa tofauti, wamewahukumu kifo ambayo kila mtu amekuwa akizungumzia. Tutakata rufaa kesho na tuone maamuzi yatakayochukuliwa.
Baadhi ya taarifa katika habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali.
Forum