Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 17:53

Sweden yaripoti kisa cha kwanza cha Mpox


Picha ya mtoto aliyeambukizwa mpox nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 19, 2024. Picha ya Reuters
Picha ya mtoto aliyeambukizwa mpox nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 19, 2024. Picha ya Reuters

Sweden Alhamisi iliripoti kisa cha kwanza cha aina ya ugonjwa unaombukiza sana wa mpox ambao kwa sasa unaendelea kusambaa eneo la Afrika ya kati na Afrika mashariki.

Kisa cha Sweden ni kisa cha kwanza cha virusi hivyo nje ya bara la Afrika.

Taarifa hiyo inajiri siku moja baada ya shirika la afya duniani WHO kuutangaza ugonjwa wa mpox kama dharura ya afya ya umma duniani baada ya mlipuko huo ulioanzia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kusambaa hadi katika nchi 12 za Afrika.

“Ni wazi kwamba jibu la pamoja la kimataifa ni muhimu kudhibiti hiyi milipuko na kuokoa maisha, mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema Jumatano.

Kundi la kimataifa linalofadhili chanjo, GAVI, limesema lina hadi dola milioni 500 za kutumia ili kupeleka chanjo katika maeneo yanayoathirika barani Afrika, shirika la habari la Reuters liliripoti Alhamisi.

Hata hivyo, zoezi la usambazaji linaweza kucheleweshwa, kwa sababu WHO lazima kwanza iidhinishe chanjo hizo, huku shirika hilo likisema linatumai kuchukua hatua hiyo ifikapo mwezi Septemba.

Forum

​
XS
SM
MD
LG