Mgomo huo utakaochukua jumla ya saa 100, ulianza saa sita mchana kwa saa za huko, na kujumuisha jumla ya wafanyakazi 350 kwenye kiwanda hicho kilichoko katika jimbo la Kusini mwa Australia. Kulingana na umoja wa wafanyakazi wa viwanda vya Australia, AMWU, kiwanda hicho huwa kinakarabati manowari aina ya Collins.
Muungano huo umeongeza kusema kuwa mgomo huo ambao ni miongoni mwa mingine iliyofanyika tangu Mei, unachelewesha ukarabati wa manowari mbili za Collins, kati ya 6 zilizopo nchini humo. Hata hivyo haijatoa maelezo kuhusu hali ya manowari hizo, kutokana na sababu za usalama wa taifa.
Wanaoshiriki mgomo huo wanadai kuna tofauti ya malipo kati ya wafanyakazi kwenye kiwanda cha Kusini mwa Australia, wale wa Magharibi. Wale wa jimbo la Kusini wanasemekana kulipwa asilimia 17.5 chini ya wenzao wa jimbo la Magharibi.
Forum