“Leo ni mwanzo mzuri,” msemaji wa White House anayehusika na masuala ya usalama wa taifa John Kirby aliwaambia waandishi wa habari.
“Bado kuna kazi nyingi ya kufanya. Kwa kuzingatia utata wa makubaliano hayo, hatutarajii kuondoka kwenye mazungumzo hayo leo na makubaliano,” aliongeza.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuendelea hadi leo Ijumaa.
Mkurugenzi wa idara ya ujasusi ya Marekani William Burns ni miongoni mwa wanaoshiriki.
Wapatanishi kutoka Marekani, Misri na Qatar walikutana na ujumbe kutoka Israel. Hamas Jumatano ilisema haitoshiriki katika mazungumzo hayo, lakini wawakilishi wake wanaweza kukutana na wapatanishi baadaye, Reuters iliripoti.
Maafisa wa afya wa Palestina wamesema zaidi ya watu 40,000 waliuawa katika operesheni za Israel za kulipiza kisasi kufuatia watu 1,200 waliouawa na Hamas na 250 kutekwa nyara na kundi hilo wakati wa shambulizi la kushtukiza la Oktoba 7.
Zaidi ya mateka 100 bado wanashikiliwa na Hamas.
Maafisa wa Palestina wanasema wengi miongoni mwa waliouawa katika vita hivyo ni wanawake na watoto, huku Israel ikisema wengi wao ni wapiganaji.
Forum