Mwanariadha wa Olimpiki kutoka Uganda, Rebecca Cheptegei aliyedaiwa kufa kutokana na ya kuchomwa na petroli na mpenzi wake wa zamani amezikwa Jumamosi kwa heshima zote za kijeshi.
Marekani Alhamisi ilitangaza msururu wa vikwazo dhidi ya serikali ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro.
Israel Alhamisi ilitangaza kwamba imefuta vibali vya uandishi wa habari kwa wanahabari wanne wa Al Jazeera wanaofanya kazi ndani ya nchi.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limeongeza kwa mwaka mwingine vikwazo vya silaha kwa pande zinazopigana katika jimbo la Darfur nchini Sudan, ambako vita kati ya majenerali hasimu vimepamba moto katika miezi ya hivi karibuni.
Mashambulizi ya anga ya Israel usiku kucha hadi Jumatano katika shule ya Umoja wa Mataifa inayowahifadhi wakimbizi wa ndani wa Palestina na kwenye nyumba mbili, yaliua watu 34 wakiwemo wanawake na watoto, maafisa waliripoti.
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, alikabiliana na mpinzani wake wa chama cha Democratic, Kamala Harris, katika mdahalo uliofanyika jana Jumanne, kuhusu masuala kama vile utoaji mimba, uhamiaji na sera za kigeni.
Russia inasema ilianzisha mazoezi makubwa ya jeshi la majini na la angani Jumanne ambayo yatafanyika kwenye eneo kubwa la bahari na kuhusisha zaidi ya meli 400 za wanamaji, ndege 120 za kijeshi na zaidi ya wanajeshi 90,000.
Wizara ya afya huko Gaza Jumanne ilisema shambulizi la kombora la Israel katika eneo lililotengwa kuhifadhi wakimbizi wa ndani katika Ukanda wa kusini mwa Gaza, liliua watu 19 na kujeruhi wengine 60.
Ufyatuaji risasi katika shule ya sekondari jimboni Georgia siku ya Jumatano ilikuwa ni ukumbusho mkubwa kwamba silaha zinawaua Wamarekani zaidi kuliko katika nchi yoyote kubwa yenye kipato cha juu, kwa mujibu wa watalaamu wa afya.
Sheria ya Huduma Nafuu ya Afya ACA ambayo pia inajulikana kama “Obamacare,” imeongeza fursa ya huduma za afya kwa mamilioni ya Wamarekani, lakini haiko bayana nini mustakabali wa program chini ya rais ajaye.
Afisa mkuu wa shirika la afya duniani Alhamisi alisema kwamba Israel imekubali sitisho la mapigano kwa saa tisa kila siku katika muda wote wa kampeni kabambe ya kutoa chanjo dhidi ya polio katika Ukanda wa Gaza, ambako kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kiligunduliwa kwa mtoto mchanga mapema mwezi huu.
Mkuu wa shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP) Jumatano alisema kwamba shirika hilo limesimamisha kwa muda usiojulikana safari za wafanyakazi wake huko Gaza, baada ya timu ya wafanyakazi wake kushambuliwa kwa risasi karibu na kituo cha jeshi la Israel siku ya Jumanne.
Israel Jumanne ilisema ilimuokoa mateka mwingine kati ya mateka 250 waliotekwa nyara na wanamgambo wa Hamas wakati wa shambulizi lao baya la mwezi Oktoba.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya kwamba wakimbizi na jamii zilizohamishwa kutoka kwa makazi yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchi nyingine za Afrika walioambukizwa mpox wako katika hatari kubwa ya ugonjwa na kifo, kwa sababu ya mazingira ambayo wanalazimika kuishi.
Kiongozi mkuu wa Iran ametangaza kwamba yuko tayari kwa mashauriano mapya na Marekani kuhusu mpango wa Iran wa nyuklia.
Russia Jumatatu ilirusha ndege zisizo na rubani 200 na makombora ndani ya Ukraine na kuua watu 4 na kusababisha umeme kukatika katika miji kadhaa nchini kote, maafisa wa Ukraine wamesema.
Jeshi la Israel Jumapili lilisema chanjo za polio zilitolewa huko Gaza kwa zaidi ya watu milioni 1, baada ya kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuthibitishwa katika eneo hilo katika kipindi cha robo karne.
Israel Jumapili mapema ilifanya shambulizi lake kubwa zaidi dhidi ya kundi la Hezbollah katika miezi 10 ya mapigano, chanzo cha usalama cha Israel kiliiambia VOA kwamba lilikuwa shambulizi la kijasusi kuzuia maelfu ya roketi na ndege zisizokuwa na rubani kurushwa kwenye ardhi ya Israel.
Mwezi mmoja tu baada ya Rais Joe Biden kutangaza hatawania tena kuchaguliwa kwa muhula mwingine, Kamala Harris alikubali uteuzi wa chama cha Democratik kuwa mgombea urais.
Juhudi za kidiplomasia kumaliza vita vya Israel na Hamas zinaboreshwa na ziara mpya ya Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken huko Mashariki ya Kati.
Pandisha zaidi