Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 22:16

Harris ataka masharti makali ya kumiliki bunduki huku Trump akiahidi kuondoa masharti


Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republikan Donald Trump (kulia) na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratic Kamala Harris.
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republikan Donald Trump (kulia) na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Demokratic Kamala Harris.

Ufyatuaji risasi katika shule ya sekondari jimboni Georgia siku ya Jumatano ilikuwa ni ukumbusho mkubwa kwamba silaha zinawaua Wamarekani zaidi kuliko katika nchi yoyote kubwa yenye kipato cha juu, kwa mujibu wa watalaamu wa afya.

Makamu Rais Kamala Harris anataka sheria kali za udhibiti wa bunduki. Mpinzani wake, Rais wa zamani Donald Trump, ameahidi kuondoa masharti ya kudhibiti bunduki.

Tukio la ufyatuaji risasi katika Shule ya Sekondari ya Apalachee. huko Winder, Georgia siku ya Jumatano ambalo limesababisha vifo vya watu kadhaa na wengine sksujeruhiwa. Makamu Rais na mgombea urais wa Democratic Kamala Harris alizungumzia tukio hilo wakati wa kampeni yake huko New Hampshire.

Shambulizi la bunduki katika shule ya sekondari huko Georgia Jumatano, Septemba 4, 2024.
Shambulizi la bunduki katika shule ya sekondari huko Georgia Jumatano, Septemba 4, 2024.

Kamala Harris, Mgombea Urais wa Democratic amesema: “Lazima tulimalize kabisa janga hili la ghasia za bunduki katika nchi yetu, unajua, haitakiwi iwe hivi.”

Suala la ghasia za bunduki nchini Marekani limeangaziwa sana katika Mkutano Mkuu wa Democratic mwaka huu

Harris aliweka mbele vipaumbele vyake katika suala hili mapema wakati wa kampeni yake.

Harris anaelezea zaidi: “Tutakaposhinda Novemba, hatimaye tutapitisha ukaguzi wa jumla, sheria inayoonyesha kuna tatizo, na marufuku kwa silaha za mashambulizi.”

Harris anasema anataka kuwepo na hatua muafaka za usalama wa bunduki na “siyo kujaribu kuwachukulia watu bunduki zao.”

Rais wa kituo cha Brady cha kuzuia ghasia za bunduki, Kris Brown, anaamini Harris atatimiza ahadi yake.

Brown ameongeza kuwa: Mgombea Harris amekuwa wazi kabisa, bayana kuwa ghasia za bunduki, ni Namba Moja katika kuwaua watoto wa Kimarekani, ni tatizo ambalo linahitaji mtizamo wa ngazi mbali mbali kulisuluhisha. Tunahitaji sera bora.”

Rais wa zamani Donald Trump alijibu tukio la ufyatuaji risasi huko Georgia kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social. Alielezea uungaji mkono wake kwa waathirika na kumuita mshambuliaji kwa maneno yake “mgonjwa na zimwi mharibifu.”

Waconservative mara kwa mara wanatetea haki za bunduki, lakini katika Mkutano Mkuu wa Republican mwaka huu haukuweka kipaumbele katika suala hili. Tukio lilifanyika mwezi Julai siku mbili baada ya Trump, mgombea urais, kulengwa kwa jaribio la kuuawa. Hilo halikubadili msimamo wake kwa Wamarekani kuwa na fursa ya kumiliki bunduki.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema: “Kama ukitaka kuchukua bunduki, huwezi kufanya hivyo. Kwasababu watu wanahitaji bunduki kujilinda.”

Trump alisimama pamoja na wamiliki wa bunduki wakati alipokuwa rais na aliahidi kuondoa masharti yaliyopitishwa na utawala wa Biden.

Makundi yanayounga mkono haki za bunduki yanasema kama wamiliki wakijitokeza kupiga kura mwezi Novemba, wanaweza kubadili mizani kwa upendeleo wao katika majimbo yenye ushindani mkali sana.

Alan Gottlieb wa taasisi ya Second Amendment Foundation anasema: Kuirudisha tena White House ili kuwa na mamlaka ya utendaji ya serikali ambayo haikiuki haki za bunduki, na katika wilaya za bunge, kuimarisha haki za bunduki katika Baraza la Wawakilishi na kupata udhibiti wa Baraza la Seneti Marekani.”

Gottlieb anaelezea, hata hivyo, kwamba haki za bunduki kihsitoria halijakuwa suala la juu katika orodha ya wasi wasi wa wapiga kura kama uchumi au uhamiaji.

Forum

XS
SM
MD
LG