Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 21:15

Mtuhumiwa wa jaribio la kumuua Trump alipokea tuzo ya Masomo Hesabu na Sayansi


Polisi wakiendelea kuweka vizuizi barabarani kuizunguuka nyumba ya Thomas Matthew Crooks. Picha na Rebecca DROKE / AFP.
Polisi wakiendelea kuweka vizuizi barabarani kuizunguuka nyumba ya Thomas Matthew Crooks. Picha na Rebecca DROKE / AFP.

Katika sherehe za mahafali 2022, Thomas Matthew Crooks aliyetajwa na FBI kuwa mshukiwa kwa kile kinachoelezewa jaribio la kumuua rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akipokea cheti cha kumaliza masomomya sekondari.

Crooks alihitimu mwaka 2022 kutoka shule ya sekondari ya Bethel Park, kulingana na Pittsburgh Tribune-Review. Alipokea “tuzo ya nyota” ya dola 500 kutoka Mpango wa Kitaifa wa Masomo ya Hesabu na Sayansi.

Maafisa wa FBI wamesema siku ya Jumapili kuwa mshukiwa alitekeleza kitendo hicho peke yake.

Idara hiyo imesema kuwa haifahamu itikadi inayohusishwa na mshukiwa au dalili zozote za matatizo ya akili au kuwahi kutoa matamshi yoyote ya vitisho katika akaunti za mitandao ya kijamii za mshukiwa huyo.

Forum

XS
SM
MD
LG