Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:24

Trump ajeruhiwa akihutubia mkutano wa kampeni Pennsylvania


Rais Donald Trump muda mfupi baada ya kujeruhiwa alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni mjini Butler, Pennsylvania.
Rais Donald Trump muda mfupi baada ya kujeruhiwa alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni mjini Butler, Pennsylvania.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alijeruhiwa Jumamosi jioni wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Butler, Pennsylvania.

Trump, ambaye ni mgombea urais mtarajiwa kwa tikiti ya chama cha Republikan, alionekana akinyoosha mkono wa kulia kuelekea shingoni mwake kabla ya shambulizi hilo kutokea.

Maafisa wa ulinzi wa rais kwa haraka walikimbilia kwenye jukwaa kujaribu na kumzingira kiongozi huyo huku hali ya wasiwasi ikionekana kutanda.

Damu ilionekana usoni mwake na kwenye sikio lake la upande wa kulia.

Vishindo viliendelea huku maafisa wakimhudumia jukwaani kabla ya kumshusa na kumpleka kwneye gari lililokuwa karibu.

Msafara wake uliondoka kwa haraka.

Katika taarifa, ofisi ya maafisa wa ulinzi wa rais ilisema "rais wa zamani Trump yuko salama."

Kampeni yake pia ilithibitisha kwamba yuko salama na alikuwa akihudumiwa katika kituo cha afya.

"Ilisikika kama milio ya risasi," mtu mmoja aliyehudhuria mkutano huo alinukuliwa na shirika la habari la Fox News akisema.

Umati wa watu ulisiskika ukimshangilia wakati akiondolewa kwenye jukwaa na kupelekwa kwa gari lake, huku akiinua mkono wake kuonyesha ishra ya ushindi.

Hayo yalijiri simu moja tu kabla ya kongamano kuu la chama cha Republican lililopangwa kufanyika kuanzia Jumatau mjini Milwauke, Wisconsin, ambapo Trump alitarajiwa kutangazwa rasmi kama mgombea urais kuelekea kwa kuchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu.

Maafisa wa usalama walinukuliwa na shirika la habari la Reuters wakisema kwamba "aliyefanya shambulizi hilo si tishio tena."

White House ilisema kwamba Rais Joe Biden alikuwa amefahamishwa kuhusu tukio hilo.

Baadaye, Biden alishutumu shambulizi hilo na kusema "vurugu za kisiasa hazikubaliki nchini Marekani."

Forum

XS
SM
MD
LG