Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, alikabiliana na mpinzani wake wa chama cha Democratic, Kamala Harris, katika mdahalo uliofanyika jana Jumanne, kuhusu masuala kama vile utoaji mimba, uhamiaji na sera za kigeni.
Ufyatuaji risasi katika shule ya sekondari jimboni Georgia siku ya Jumatano ilikuwa ni ukumbusho mkubwa kwamba silaha zinawaua Wamarekani zaidi kuliko katika nchi yoyote kubwa yenye kipato cha juu, kwa mujibu wa watalaamu wa afya.
Kinyume na ilivyo katika nchi nyingine, Marekani haina sheria ya ukomo wa muda maalum wa kampeni za urais.
Baadhi ya familia za Gold Star zimeelezea uungaji mkono wao Jumapili kwa rais wa zamani Donald Trump, baada ya kukosolewa kwa kupiga picha na video katika sehemu iliyowekewa kizuizi kwenye Makaburi ya Kitaifa ya Arlington wiki iliyopita.
Kamala Harris ameahidi kuchukua msimamo mkali juu ya uhamiaji katika eneo la mpaka wa kusini wa Marekani na kusema hatozuia upelekaji silaha kwa Israel.
Sheria ya Huduma Nafuu ya Afya ACA ambayo pia inajulikana kama “Obamacare,” imeongeza fursa ya huduma za afya kwa mamilioni ya Wamarekani, lakini haiko bayana nini mustakabali wa program chini ya rais ajaye.
“Alikuwa ni malkia wa mpakani. Mara ghafla anasema yeye siyo tena malkia wa mpakani,” alisema Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Mwezi mmoja tu baada ya Rais Joe Biden kutangaza hatawania tena kuchaguliwa kwa muhula mwingine, Kamala Harris alikubali uteuzi wa chama cha Democratik kuwa mgombea urais.
Gavana wa Minnesota Tim Walz Jumatano usiku amekubali rasmi uteuzi wa chama chake kugombea nafasi ya makamu wa rais.
Obama alikuwa mzungumzaji mkuu katika usiku wa pili wa mkutano mkuu wa chama huko Chicago.
Kufuatia kujiondoa kwa Rais Joe Biden katika kinyang’anyiro cha urais, mtizamo wa Chama cha Demokratik umejikita katika mkutano mkuu wa uteuzi wa wagombea.
Warepublican katika Bunge wanaunga kwa karibu na mgombea urais Donald Trump katika masuala kadhaa muhimu ya sera ya mambo ya nje ikiwa ni pamoja na uungaji mkono wa Marekani kwa Israel.
Pandisha zaidi