Jeshi la Israel lilisema ndege zake za kivita 100 zilishambulia zaidi ya maeneo 40 yanayotumiwa na Hezbollah kwa kurusha maelfu ya maroketi na ndege zisizokuwa na rubani kusini mwa Lebanon muda mfupi kabla ya saa tano saa za huko.
Hezbollah ilitajwa na Marekani kama kundi la kigaidi na ni kundi kubwa linaloungwa mkono na Iran katika kanda hiyo.
Saa kumi na nusu alfajiri, Hezbollah ilianza kufyatua zaidi ya maroketi 150 na ndege zisizokuwa na rubani ndani ya eneo la kaskazini mwa Israel. Mwanajeshi mmoja wa Israel aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi hayo, ambayo yaliharibu baadhi ya majengo, jeshi la Israel lilisema.
Katika msururu wa taarifa kwenye mtandao wa kijamii, Hezbollah ilisema ilirusha zaidi ya maroketi 300 na ndege zisizokuwa na rubani ndani ya Israel nyakati za alfajiri kama sehemu ya kile imekielezea kama ulipizaji kisasi dhidi ya mauaji ya kamanda wake mkuu, Fouad Shukur, yaliyofanywa na Israel kusini mwa Beirut tarehe 30 Julai.
Forum