Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 22:17

Hotuba ya Kukubali Uteuzi: Harris atoa mtizamo dhidi ya mpinzani wake Trump


APTOPIX Election 2024 DNC
APTOPIX Election 2024 DNC

Mwezi mmoja tu baada ya Rais Joe Biden kutangaza hatawania tena kuchaguliwa kwa muhula mwingine, Kamala Harris alikubali uteuzi wa chama cha Democratik kuwa mgombea urais.

Alielezea rekodi yake na mtizamo wake dhidi ya mpinzani wake wa Republican, Rais wa zamani Donald Trump.

Ukipambwa kwa maonyesho ya muziki usiku wa mwisho wa mkutano mkuu wa chama cha Democratic, ilikuwa ni pamoja na mwanamuziki Pink, na wimbo wa taifa ulioimbwa na kundi la country The Chicks.

Lakini Kamala Harris alikuwa ni nyota katika usiku huo.

Kamala Harris, Mgombea Urais wa Democratic: “Kwa niaba ya kila mtu ambaye hadithi yake inaweza tu kuandikwa katika taifa hili adhimu, nakubali uteuzi wenu kuwa rais wa Marekani.”

Harris alielezea hadithi binafsi ya maisha yake, akihusisha nay ale waliyopitia wapiga kura wa daraja la kati.

Mkutano wa Wademokratik wa Kitaifa (DNC) huko Chicago
Mkutano wa Wademokratik wa Kitaifa (DNC) huko Chicago

Kamala Harris, Mgombea Urais wa Democratic anasema: “Tunafungua njia mpya ya kusonga mbele. Mbele kwa mustakbali wenye nguvu na kukua kwa daraja la kati, kwasababu tunafahamu kuwa daraja la kati lenye nguvu siku zote ni muhimu sana kwa mafanikio ya Marekani na kujenga daraja la kati itakuwa ni lengo kuu katika urais wangu.”

Aliangazia kazi ujuzi wake kama mwendesha mashtaka wa zamani,

Kulinganana na mkakati wa chama chake dhidi ya mgombea wa Republican Donald Trump, ambaye amekutwa na hatia mahakamani.

Kama walivyokuwa wasemaji wengine wengi, alionya juu ya nyaraka zinazoelezea msimamo mkali wa sera za mrengo wa kulia zinazohusishwa na Trump. Rais wa zamani alikanusha hili.

Kamala Harris, Mgombea Urais wa Democratic anaeleza: “Tunafahamu fika awamu ya pili ya uongozi wa Trump itakuwaje. Yote yameelezwa kwenye Project 2025, iliyoandikwa na washauri wake wa karibu sana, na inahitimisha kwa jumla ni kuirudisha nyuma nchi yetu kwenye siki zilizopita. Lakini Marekani, haturejei nyuma.”

Ndani ya ukumbi ilikuwa ni nderemo. Nje, kulikuwa na maandamano yanayowaunga mkono Wapalestina, yalifanyika kila siku,

Maandamano hayajateteresha msimamo wa Harris kuhusu vita huko Gaza. Wakati alisisitiza umuhimu wa ulinzi na misaada kwa Wapalestina, alielezea tena uungaji mkono kwa Israel kujilinda. Alitaka sitisho la haraka la mapigano na njia ya kuwa na sulusho la mataifa mawili.

Maandamano ya kuunga mkono Wapalestina yakifanyika huko Chicago wakati wa Mkutano wa Wademokratik wa Kitaifa (DNC) in Chicago, Illinois, Aug. 22, 2024.
Maandamano ya kuunga mkono Wapalestina yakifanyika huko Chicago wakati wa Mkutano wa Wademokratik wa Kitaifa (DNC) in Chicago, Illinois, Aug. 22, 2024.

Gaza ni moja ya eneo ambalo Wademocrat hawakubaliani. Kati ya wajumbe 4,700, 270 wametia saini waraka kuitaka Marekani iache kuwapatia silaha Israel.

Hotuba ya Harris kwa taifa imekuja mwezi mmoja tu baada ya Rais Joe Biden kutangaza hatawania kuchaguliwa tena.

Kamala Harris, Mgombea Urais wa Democratic anasema: “Joe, nimejawa na shukrani. Rekodi yako si ya kawaida, kama historia itakavyoonyesha, na tabia yako inatia hamasa, na Doug nakupenda na Jill, na siku zote nitakuwa mwenye kuwashukuru nyote.”

Wakati Harris alipokuwa akizungumza, Trump alitaka kurudisha mtizamo kwake kwa kuutembelea mpaka wa Marekani na Mexico na kuwa mwenyeji katika tukio kwenye mtandao wa kijamii.

Mgombea urais wa Republikan Donald Trump akiongea katika mpaka wa kusini mkabala na Mexico, huko Sierra Vista, Arizona, Agosti. 22, 2024.
Mgombea urais wa Republikan Donald Trump akiongea katika mpaka wa kusini mkabala na Mexico, huko Sierra Vista, Arizona, Agosti. 22, 2024.

Lakini hakuna kilichopunguza shauku ya wajumbe.

Darrell Bakeman, Mjumbe kutoka Arizona alisema: “Anatutengenezea mustakbali wa siku zijazo, wakati ujao ambao tumekuwa tukiusubiri, ambao unamuwakilisha kila mtu katika nchi hii, tunafuraha kwmaba muovu hana nguvu na sisi tunasonga mbele na maisha mazuri.”

Sam Hudis, Mjumbe kutoka New York anasema: “Kamala alielezea kwa hakika nini ambacho kiop hatarini kwa nchi hii. Sote tunapeperusha bendera ya Marekani, Sote tunayo USA, hiyo ni kwasababu. Kwa vile hapa ni mapambano kwa ajili ya nchi hii.”

Mgombea mwenza Tim Waltz alijiunga na Harris jukwaani kufunga mkutano mkuu, huku zikiwa zimebaki siku 74 tu mpaka siku ya uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG