Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 00:41

Russia na China zaanzisha mazoezi makubwa ya kijeshi


Picha hii inaonyesha meli za kijeshi za China na Russia zikishiriki katika mazoezi ya pamoja kwenye bahari ya kusini mwa China, Disemba 27, 2022.
Picha hii inaonyesha meli za kijeshi za China na Russia zikishiriki katika mazoezi ya pamoja kwenye bahari ya kusini mwa China, Disemba 27, 2022.

Russia inasema ilianzisha mazoezi makubwa ya jeshi la majini na la angani Jumanne ambayo yatafanyika kwenye eneo kubwa la bahari na kuhusisha zaidi ya meli 400 za wanamaji, ndege 120 za kijeshi na zaidi ya wanajeshi 90,000.

Mazoezi hayo ya kijeshi yaliyopewa jina la “Ocean 24,” yanahusisha wanajeshi wa China na yatafanyika hadi tarehe 16 Septemba, na takriban nchi 15 zimealikwa kufuatilia mazoezi hayo, kulingana na wizara ya ulinzi ya Russia.

Rais wa Russia Vladimir Putin alisema Russia “inakuwa makini sana” katika kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na “nchi rafiki” na aliionya Marekani kutojaribu kuiondoa Moscow huko Asia.

Wachambuzi wanasema mazoezi hayo ya pamoja ni juhudi za Russia na China kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kukabiliana na ushirikiano mkubwa wa pamoja wa kiusalama kati ya Marekani na washirika wake katika kanda ya Indo-Pacific.

Forum

XS
SM
MD
LG