Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 11:58

Ziara ya Blinken Mashariki ya Kati yaboresha juhudi za kumaliza vita vya Israel na Hamas


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili Tel Aviv Agosti 18, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili Tel Aviv Agosti 18, 2024.

Juhudi za kidiplomasia kumaliza vita vya Israel na Hamas zinaboreshwa na ziara mpya ya Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken huko Mashariki ya Kati.

Lakini wakati matumaini ya sitisho la mapigano yakiwa juu, utekelezaji huenda ukathibitisha ukawa na changamoto, wachambuzi wanasema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amerejea Mashariki ya Kati katika msukumo mpya wa kupatikana kwa sitisho la mapigano katika vita vya Israel na Hamas.

Kumaliza vita huenda kukafanyika katika awamu tatu, anaelezea profesa wa masuala ya usalama wa taifa katika chuo kikuu cha New Haven, Howard Stoffer.

Howard Stoffer, Mtaalamu wa Usalama wa Taifa anaeleza: “Awamu ya kwanza itakuwa na kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kutoka kwenye maeneo muhimu huko Gaza, kuacha kwa mapigano. Halafu itakuwa ni kubadilishana baadhi ya matekani, mateka walio hai, wanawake, wazee na waliojeruhiwa, na kutakuwa na baadhi ya wafungwa wa Palestina ambao watarejeshwa kwa Hamas.”

Utekelezaji huenda ukathibitika ukawa na ugumu, Stoffer anaelezea zaidi: “Huenda kukawa na tofauti ya maoni kuhusu nani huenda akaachiliwa. Na mchakato wa kuondoka hata kutoka Gaza una mkanganyiko kwasababu Netanyahu, waziri mkuu wa Israel amesema kwamba wanataka masharti kwa watu binafsi wenye silaha kusini mwa Gaza kuingia Gaza Kaskazini.”

Ziara ya Blinken inakuja huku mivutano ikiwa juu mno. Iran huenda bado ikapiliza kisasi kwa mauaji ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh mwezi uliopita mjini Tehran. Mazungumzo ya amani yenye mafanikio huenda yakatuliza hali.

Howard Stoffer, Mtaalamu wa Usalama wa Taifa anasema: “Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba Hezbollah yenyewe, au Iran na Hezbollah watafanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Israel. Kama wakifanya hivyo, kutakuwa na vita vipana zaidi katika eno zima.”

Iran inafanya mazoezi ya kijeshi kama inavyoonyesha picha hii iliyotolewa na tovuti rasmi ya jeshi la Iran Ijumaa, Januari 19, 2024.
Iran inafanya mazoezi ya kijeshi kama inavyoonyesha picha hii iliyotolewa na tovuti rasmi ya jeshi la Iran Ijumaa, Januari 19, 2024.

Kumalizika kwa vita huenda kukahakikisha usambazaji wa misaada ya kibinadamu huko Gaza na kuruhusu chanjo ya wengi dhidi ya kuongezeka kwa tishio la ugonjwa wa polio. Waziri wa afya wa Palestina amethibitisha kesi ya Jumamosi. Baadhi ya kina mama wa Kipalestina wana wasi wasi.

Elham Nassar, Mama wa Kipalestina anaeleza: “Tunahitaji chanjo ya polio, tunahitaji dawa, tunahitaji huduma bora za usafi, tunahitaji kujioko kabla haijachelewa sana, au tunatakiwa kusubiri kwa muda gani? Je tusubiri mpaka tuwaone watoto wetu wakifariki au kupooza na halafu hatuna njia ya kuwasaidia kuwafanyia chochote?”

Nchini Israel, jamaa wa mateka wanaoshikiliwa na Hamas, wameelezea matumaini yao kwa tahadhari kuhusu matarajio ya sitisho la mapigano na kuachiliwa kwa wapendwa wao.

Yair Moses, Ndugu wa Mateka anaeleza: “Tumejifunza kutokana na tuliyoshuhudiakabla kutokuwa na matarajio sana kwasababu huenda makublaiano yasifikiwe, masikitisho ni makubwa mno na haraka sana unakuwa huna raha, hadi sasa hilo ni ngumu sana kulipandisha tena. Lakini bado tunajaribu kuwa na hali ya matumaini na imani.”

Hata wakati mashauriano ya amani yanayosimamiwa na Marekai, Qatar na Misri yanatarajiwa kuanza tena mjini Cairo wiki hii, operesheni za kijeshi za Israel hazijasita. Jumapili mamlaka ya Palestina iliripoti watu takriban 28 waliuawa katika mashambulizi ya usiku kucha kote Gaza. Jeshi la Israel limesema limewaua wanamgambo 20 katika mashambulizi ya Jumamosi usiku mpaka Jumapili.

Katika mkesha wa mkutano huu na Blinken, Benjamin Netanyahu aliongoza kikao cha baraza la mawaziri siku ya Jumapili ambapo alikosoa mwelekeo wa Hamas kwa mazungumzo ya amani na kurejea msimamo wake kwamba “hatua kali za kijeshi na shnikizo la kidiplomasia ndiyo njia ya kuachiliwa kwa mateka wa Israel.”

Forum

XS
SM
MD
LG